` MISA TANZANIA YAISHUKURU KAMPUNI YA ALLY'S STAR BUS KWA HUDUMA BORA NA KUSAFIRISHA WANACHAMA WAKE MKOANI IRINGA

WANDAMAN HOTEL

MISA TANZANIA YAISHUKURU KAMPUNI YA ALLY'S STAR BUS KWA HUDUMA BORA NA KUSAFIRISHA WANACHAMA WAKE MKOANI IRINGA


Na. Mwandishi wetu, Mwanza

Taasisi ya Vyombo vya Habari Kusini Mwa Afrika, (MISA TAN) imeishukuru kampuni ya Mabusi ya Ally's Star kwa huduma zake nzuri zenye viwango vya kimataifa.

Mwenyekiti wa MISA Tan Bwana Edwin Soko ametoa shukrani hizo za dhati kupitia kwa Meneja wa Kampuni ya Mabusi hayo Bwana Ally Salumu

Soko amesema kuwa, pongezi hizo sio za kusikia juu ya huduma bora za Allys bali za kujionea kwani Kampuni hiyo iliwasafirisha wahariri na waandishi wa habari ambao ni wanachama wa MISA Tan waliotoka Mikoa ya Simiyu, Mara, Mwanza na Shinyanga kuelekea mkoani Iringa kuhudhuria Mkutano wa MISA Wadau Summit 2026 na Mkutano mkuu wa MISA Tan ambapo walijionea uhakika wa safari pamoja na usalama wao kwa muda wote wa safari.

Soko ameongeza kuwa, Ally's Bus walitoa huduma nzuri na kwa viwango bora kwa waandishi wa habari hao ikiwemo kuwapa punguzo la bei kwa kutambua mchango wa waandishi wa habari kwenye sekta ya usafirishaji, viburudisho na burudani kwa mufa wote wa safari.

Soko amewahakikishia watanzania kwa ujuma kuendelea kusafiri na Busi za Ally's kwa safari zao za kila siku .

Pia amemahukuru Meneja Ally Salumu kwa kuiamini Taasisi ya MISA Tanzania kwa kukubali kufanya nao kazi kwa moyo mkunjufu.
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464