TFS SHINYANGA KUANZISHA UTALII WA IKOLOJIA HIFADHI YA MSITU WA LUBAGA
Na Marco Maduhu, SHINYANGA
Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) Wilaya ya Shinyanga wanatarajia kuzindua utalii wa ikolojia katika hifadhi ya Msitu wa Lubaga maarufu Harsh ifikapo Julai mwaka huu.
Utalii huo utahusisha shughuli mbalimbali ikiwamo kupiga picha, kupumzika pamoja na kufanyika kwa hafla kama harusi na sherehe nyingine.
Akizungumza na waandishi wa habari leo Marchi 20,2026 katika hifadhi hiyo, Ofisa Mwandamizi wa Uhifadhi kutoka TFS Wilaya ya Shinyanga Fabian Balele, amesema maandalizi ya kuanzisha huduma hizo yanaendelea.
Amesema hifadhi hiyo ina vivutio vya asili vinavyovutia utalii wa ikolojia, hivyo wameanza kuweka miundombinu ya msingi kwa ajili ya shughuli hizo.
“Hapa kutakuwa na utalii wa ikolojia ukiwamo kupiga picha, kupumzika na kumbi za mikutano ya nje kwa ajili ya hafla mbalimbali zikiwamo harusi. Pia kutakuwa na njia ya kuendesha baiskeli yenye urefu wa kilomita saba, na tunatarajia kuanzisha bustani ya wanyama,” amesema Balele.
Aidha, amesema watalii watakaotembelea eneo hilo watapatiwa elimu ya uhifadhi wa misitu na ufugaji nyuki ili kusaidia kulinda mazingira.
MAELEZO KATIKA PICHA👇👇
Ofisa Mwandamizi wa Uhifadhi kutoka TFS Wilaya ya Shinyanga Fabian Balele akizungumza.
Ofisa Mwandamizi wa Uhifadhi kutoka TFS Wilaya ya Shinyanga Fabian Balele akizungumza.
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464