NAIBU KATIBU MKUU UVCCM, MWAKITINYA ATAJA MAFANIKIO SIKU 100 ZA RAIS DKT. SAMIA
Naibu Katibu Mkuu wa UVCCM, Ndugu Mussa P. Mwakitinya (MNEC) amempongeza Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kutimiza kwa asilimia kubwa aliyoahidi kuyafanya katika siku 100 za kwanza za uongozi wake kwa Watanzania.
Ndugu Mwakitinya akizungumza jana Januari 24, 2026 katika Ukumbi wa Chuo cha Maendeleo ya Jamii (CDT) Monduli mkoani Arusha katika Campus Life Kick Off amesema bado siku 100 hazijafika ila wananchi wameona matunda na inaonyesha Rais Dkt. Samia anavyowapenda Watanzania.
Ametaja mafanikio hayo kuwa tayari zimetolewa ajira 7,000 na nyingine 5,000 na watumishi wapya washaripoti kazini, Bima ya Afya kwa wote ambayo imeshatangazwa kufanya kazi kwa kila kaya kuchangia Shilingi 150,000.
"Rais Dkt. Samia wakati anaingia madarakani alikuta Bodi ya Mikopo inatoa Shilingi bilioni 458 akasema haziwatoshi vijana wangu, akaongeza hadi Bilioni 570 akasema hapana akaongeza hadi Bilioni 650 akasema bado haziwatoshi akaongeza Bilioni 787 mama akasema bado haziwatoshi awamu hii ameongeza hadi Bilioni 915.6," amesema Ndugu Mwakitinya
Pia amepongeza mpango wa Serikali kupitia PPRA kuzifanya Taasisi zote kutenga asilimia 30 ya zabuni kupewa vikundi ikiwemo Vijana ili kufanikiwa kuwa mabilionea wa baadae.
#kazinaututunasongambele
#fyuchabilastresi
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464



