Na Marco Maduhu, SHINYANGA
WANANCHI wa Kata ya Isaka Halmashauri ya Msalala wilayani Kahama, wameeleza kuupokea kwa furaha mradi wa ukarabati wa reli ya kati, ambao utafungua fursa za ajira, kukuza biashara na kuimarisha uchumi wa eneo hilo.
Wamebainisha hayo jana wakati Maafisa kutoka Shirika la Reli Tanzania (TRC) walipokuwa wakiwapatia elimu ya uelewa kuhusu utekelezwaji wa mradi ukarabati wa reli hiyo ya kati kwa awamu ya pili kutoka Dar es Salaam hadi Isaka, utakaoanza kutekelezwa mwezi Aprili 2026 hadi 2029.
Mmoja wa wananchi hao Said Hamadi, amesema wanaishukuru serikali kwa kuendelea kutekeleza miradi ya kimkakati, ambayo imekuwa chachu ya maendeleo kwa wananchi, kwa kupata fursa mbalimbali zikiwamo ajira, kukuza biashara na kuinuka kiuchumi.
“Sisi wananchi wa Isaka tumeupokea mradi huu wa ukarabati wa reli ya kati kwa mikono miwili, ila nawaomba mkandarasi ambaye atatekeleza mradi huu, atoe kipaumbele cha ajira kwa vijana wa hapa Isaka na tupo tayari kushirikiana naye,” amesema Hamadi.
Naye Diwani wa Kata ya Isaka Pazi Majuto, amesema mradi huo ni fursa kubwa kwa wananchi wa Isaka, na kwamba mji huo sasa una kwenda kuwa kitovu kikubwa cha uchumi, sababu maeneo hayo pia kuna bandari kavu na reli hiyo inafaida ya usafirishaji mizigo.
“Kwa niaba pia ya wananchi wote wa Isaka, mimi kama mwakilishi wao Mheshimiwa Diwani, mradi huu wa ukarabati wa reli ya kati tumeopokea kwa mikoni miwili, na Isaka sasa ina kwenda kuwa kitovu kikubwa cha uchumi, sababu miradi mingi ya kimkakati ipo hapa, na tupo tayari kwa mradi huu,” amesema Pazi.
Awali, Mhandisi wa Mradi kutoka TRC Aikande Munuo, akizungumza na wananchi wa Isaka, amesema ukarabati wa reli hiyo ya kati kutoka Dar es salaam hadi Isaka, urefu wake ni kilomita 392.4, na kwamba eneo kubwa la ukarabati awamu ya pili ni kipande cha kutoka Tabora hadi Isaka, na gharama zake ni dola za marekani milioni 200 sawa na bilioni 500 za kitanzania, mkopo kutoka benki ya dunia.
Amesema, utekelezwaji wake unategemea kuanza mwezi April hadi May mwaka huu na kukamilika mwaka 2029, ambapo kwa sasa Shirika lipo katika hatua za kumtafuta Mkandarasi, na kwamba lengo kubwa la ukarabati wa reli hiyo ni kukuza uchumi kupitia sekta ya usafirishaji.
Amesema, mradi huo wanautekeleza pia kwa kushirikiana na Tume ya Taifa ya Umwagiliaji (NIRC), ambapo yatajengwa makaravati na madaraja 171, kujengwa mabwawa sita maeneo ya Kilosa, ili kupunguza kasi ya maji na athari za mafuriko kwenye miundombinu ya reli.
“Mradi huu utakuwa na fursa nyingi kwa wananchi, ambapo kwa upande wa ajira sisi TRC hatuajiri, lakini tutamsimamia Mkandarasi kuajiri watu wa maeneo husika na mradi, fursa zingine ni kuchochea ukuaji wa biashara kwenye maeneo ambayo mradi unatekelezwa, ukuaji wa uchumi wa mtu mmoja mmoja na taifa kwa ujumla.
“Urahisi wa usafiri na usafirishaji wa abiria na mizigo kwa watumiaji wa reli ya kati, upatikanaji wa maji ya umwagiliaji kwa wakulima kupitia mabwawa, na kupata pia maji ya mifugo kwa wafugaji kwenye maeneo ya mradi,” amesema Munuo.
Naye Afisa Jamii kutoka TRC Lightness Mngulu, amewataka waanchi wa Isaka na maeneo yote ambayo mradi huo unatekelezwa kuchangamkia fursa za kiuchumi.
Afisa Usalama mradi wa Reli ya kati kutoka TRC Justine Kalokola, amewataka wananchi kwamba wakati wa utekelezwaji wa mradi huo, wailinde miundombinu, pamoja na kuzingatia usalama wao, licha ya wao kuweka ishara za usalama ili kuepuka ajali.
Mwanasheria kutoka TRC Jane Kassanda, alitoa tahadhari kwa wananchi ambao siyo waaminifu, kwa kutaja makosa na adhabu zake kwamba mtu ambaye atahujumu miundombinu ya reli na kuhatarisha usalama wa treni na abiria, watatozwa faini ya mamilioni pamoja na kufungwa jela, huku akionya pia utoaji wa rushwa kwa wananchi ili kupata ajira kwenye mradi huo.
Kwa upande wake Mkuu wa Kituo cha Polisi Tabora Hadija Salimu, amewasihi wananchi wawe wazalendo wakati wa utekelezwaji wa mradi huo, kwa kuulinda na kutofanya uharibifu wa miundombinu yake.
TAZAMA PICHA👇👇
Mhandisi wa Mradi kutoka TRC Aikande Munuo akizungumza.
Mhandisi wa Mradi kutoka TRC Aikande Munuo akizungumza.
Mhandisi wa Mradi kutoka TRC Aikande Munuo akizungumza.
Afisa Jamii kutoka TRC Lightness Mngulu akizungumza.
Afisa Jamii kutoka TRC Lightness Mngulu akizungumza.
Afisa Jamii kutoka TRC Lightness Mngulu akizungumza.
Mwanasheria kutoka TRC Jane Kassanda akizungumza.
Mwanasheria kutoka TRC Jane Kassanda akizungumza.
Mwanasheria kutoka TRC Jane Kassanda akizungumza.
kuu wa Kituo cha Polisi Tabora Hadija Salimu akizungumza.
Afisa Usalama mradi wa Reli ya kati kutoka TRC Justine Kalokola akitoa elimu ya salama wakati wa utekelezaji wa ukarabati wa reli ya kati.
Afisa Usalama mradi wa Reli ya kati kutoka TRC Justine Kalokola akitoa elimu ya salama wakati wa utekelezaji wa ukarabati wa reli ya kati.
Afisa Usalama mradi wa Reli ya kati kutoka TRC Justine Kalokola akitoa elimu ya salama wakati wa utekelezaji wa ukarabati wa reli ya kati kwa kuonyesha alama za usalama.

Afisa Usalama mradi wa Reli ya kati kutoka TRC Justine Kalokola akitoa elimu ya salama wakati wa utekelezaji wa ukarabati wa reli ya kati kwa akionyesha alama za usalama.
Mhandisi wa Mradi kutoka TRC Aikande Munuo akionyesha alama za usalama.

Diwani wa Isaka Pazi Majuto akizungumza.