Na Marco Maduhu, SHINYANGA
NAIBU Waziri wa Nishati na Mbunge wa Vitimaalumu mkoani Shinyanga Salome Makamba, amefanya ziara kutembelea miradi ya nishati ya umeme katika kituo cha kupoza umeme cha Ibadakuli Manispaa ya Shinyanga, na mradi wa umeme Jua ulipo Kijiji cha Ngunga wilayani Kishapu.
Amefanya ziaya hiyo leo Januari 9,2026 akiwa ameambanatanna viongozi mbalimbali wa serikali pamoja na chama, na kumpongeza Rais Dk.Samia Suluhu Hassan kwa uwekezaji huo mkubwa.
Akizungumza mara baada ya kutembelea miradi hiyo, amempongeza Rais Dk.Samia Suluhu Hassan, kwa uwekezaji mkubwa wa miradi hiyo ya nishati, na kwamba nchi itazalisha umeme mwingi sana, na kutakuwa na umeme wa kutosha, uhakika na wanaweza kuuza hata nchi jirani.
“Leo nimeshuhudia uwekezaji mkubwa sana wa nishati ya umeme, mbapo nchi tutazalisha umeme mwingi, na tutakuwa na umeme wa uhakik, ambao tunaweza kuuza hata nchi za jirani kama Uganda, Kenya na utatoa huduma pia kwenye mradi wa SGR,” amesema Makamba.
Aidha, ameagiza kuwa katika utekelezaji wa miradi hiyo wazawa wapewe kipaumbele cha ajira hususani vijana ambao wanazunguka eneo la mradi, ili wapate kunufaika nao na kujikwamua kiuchumi.
“Nataka kuona vijana wengi wa Shinyanga wakipata ajira kwenye utekelezaji wa miradi hii ya nishati ya umeme, na hili siyo ombi ni takwa la kisheria,” amesema Makamba.
Ametoa wito pia kwa vijana ambao wamekuwa wakipata ajira kwenye miradi hiyo kwamba, wafanye kazi kwa uaminifu na kutanguliza uzalendo na siyo kujihusisha na wizi wa vifaa vya ujenzi.
Mwenezi wa CCM Mkoa wa Shinyanga Richard Masele, naye amemshukuru Rais Samia kwa uwekezaji huo wa nishati ya umeme na kwamba utachochea ukuaji wa uchumi na kuvutia wawekezaji.
Kaimu Mkurugenzi msimamizi wa miradi TANESCO Makao Makuu Mhandisi Frank Mashalo, amesema mradi huo wa upanuzi wa kituo cha kupoza umeme cha Ibadakuli, unatekelezwa na serikali kwa asilimia 100, na mradi umefika asilimia 43 ya utekelezaji na gharama zake ni bilioni 25.
Naye msimamizi wa umeme Jua Mhandisi Emmanuel Anderson, amesema umefikia asilimia 89 ya utekelezaji katika awamu ya kwanza, kwa kuzalisha Megawati 50, na kwamba wameajiri vijana wazawa 560, na wanaotoka kijiji cha Ngunga kwenye eneo la mradi ni 67.
TAZAMA PICHA👇👇
Naibu Waziri wa Nishati Salome Makamba akizungumza.
Naibu Waziri wa Nishati Salome Makamba akizungumza.
Kaimu Mkurugenzi msimamizi wa miradi TANESCO Makao Makuu Mhandisi Frank Mashalo.
msimamizi wa umeme Jua Mhandisi Emmanuel Anderson akizungumza.
Mwenezi wa CCM Mkoa wa Shinyanga Richard Masele akizungumza.
Katibu wa Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini Samweli Jackson akizungumza.
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464