Na Marco Maduhu,SHINYANGA
MEYA Mpya wa Mansipaa ya Shinyanga Salum Kitumbo, amewataka Madiwani na Wataalamu wa Manispaa hiyo kufanya kazi kwa weledi na kuhakikisha wanatatua kero mbalimbali za wananchi na kupeleka tabasamu kwao.
Amebainisha hayo leo Desemba 4,2025 wakati akizungumza kwenye kikao cha Baraza la Madiwani wa Manispaa hiyo, mara baada ya kuchaguliwa kwa kishindo kuwa Meya, huku Pendo Sawa akichaguliwa kuwa Naibu Meya.
Amesema, matamanio ya wananchi wa Manispaa hiyo ni makubwa kwao mara baada ya kuwachangua kwenye Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29, na kwamba kazi iliyobaki ni kuwatumikia kwa kutatua kero zao mbalimbali.
“Madiwani tukatende haki kwa wananchi, na kuwatumikia ipasavyo kwa kupeleka tabasamu kwao na kutatua kero mbalimbali ikiwamo za ubovu wa barabara,ukosefu wa maji na umeme,”amesema Kitumbo.
Aidha, amesisitiza pia suala la mikopo ya Halmashauri ya Asilimia 10 kwamba ifike kwa walengwa husika ,pamoja na kusimamia urejeshwaji wa mikopo hiyo.
Naye Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga Alexius Kagunze, akizungumza kwenye mkutano huo wa Baraza la Madiwani ameahidi kushirikiana na madiwani kwa kufanya kazi ya kusukuma maendeleo ya manispaa hiyo.
TAZAMA PICHA👇👇
Meya mpya wa Manispaa ya Shinyanga Salum Kitumbo akizungumza.
Meya mpya wa Manispaa ya Shinyanga Salum Kitumbo akizungumza.
Naibu Meya wa Manispaa ya Shinyanga Pendo Sawa akizungumza.
Meya mpya wa Manispaa ya Shinyanga Salum Kitumbo (kulia)akiwa na Naibu Meya Pendo Sawa.
Mkurugenzi wa Manispaa ya Shuinyanga Alexius Kagunze akizungumza.
Katibu Tawala wa Wilaya ya Shinyanga Said Kitinga akitangaza matokeo.
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464