Na Marco Maduhu, SHINYANGA
DIWANI wa Puni Halmashauri ya ya wilaya ya Shinyanga Mhandisi Jumanne Rajabu, amefanya mkutano wa hadhara wa kuwashukuru wananchi, kwa kumchagua katika Uchaguzi Mkuu uliofanyika Oktoba 29 mwaka huu, huku akitaja vipaumbele vyake sita atakavyoanza navyo katika kipindi chake cha uongozi.
Amefanya Mkutano huo leo Desemba 13,2025 katika Kijiji cha Nyanshimbi, kwenye viwanja vya shule ya Msingi Kingwang’ona ulioandaliwa kwa lengo la kuwashukuru wananchi kwa kura nyingi walizompa yeye pamoja na Rais Dk. Samia Suluhu Hassan, na Mbunge wa Itwangi Azza Hillal Hamad.
Amesema, amefanya mkutano huo kwa ajili ya kuwashukuru wananchi wa Kijiji cha Nyanshimbi, ambapo atazunguka katika vijiji vyote vya Kata ya Puni kuwa shukuru, kutokana na kumpigia kura nyingi za ushindi pamoja na Rais Samia Suluhu Hassan, na Mbunge wa Itwangi Azza Hillal Hamad, na kwamba ahadi yake kwao ni kuwaletea maendeleo ya kweli.
"Nimekuja kusema asante kwa wananchi wa Kijiji cha Nyanshimbi, kwa kunipigia kura nyingi za ushindi kwenye Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29, na Rais wetu Samia Suluhu Hassani na Mbunge wetu Azza Hillal Hamad asanteni sana,"amesema Mhandisi Rajabu.
Aidha, ametaja vipaumbele vyake sita ambavyo ataanza navyo kwenye uongozi wake, katika kuwahudumia wananchi wa Kijiji cha Nyanshimbi, kuwa ni kutatua kero ya maji, barabara korofi, na ukosefu wa umeme ngazi ya vitongoji.
Kero zingine ni kuboresha miundombinu ya elimu, na kuhamasisha wazazi kuchangia chakula shuleni, ambapo yeye atakuwa wa kwanza kuchagia, ili watoto wasisome na njaa.
Nyingine ni kuongezeka kwa watumishi wa Zahanati kutoka wawili,ili waendane na idadi ya wananchi na kutoa tiba kwa wakati, pamoja na upatikanaji wa vifaa tiba.
Amemalizia na kipaumbele kingine cha kufufua Josho la Ng'ombe, ili wafugaji wapate mahali kuogeshea dawa mifugo yao, na kwamba kijiji hakiwezi kuwa na maendeleo kama hakuna wafugaji bora na wakulima.
"Mambo makubwa yanakuja hapa Nyanshimbi, na maendeleo ni hatua kwa hatua," amesema Mhandisi Rajabu.
Katika hatua nyingine, amewasihi wananchi waendelee kudumisha Amani ya nchi, na wasikubali kutumika kuivuruga sababu vita ni adui wa maendeleo.
Naye Katibu wa Siasa na Uenezi (CCM) Mkoa wa Shinyanga Richardi Masele, amewapongeza wananchi hao kwa kumpigia kura nyingi za ushindi Rais Dk. Samia Suluhu Hassan, Mbunge wa Itwangi Azza Hillal Hamad na Diwani wa Puni Mhandisi Jumanne Rajabu.
"Kwakuchagua mafiga haya matatu, wananchi tarajieni mvua kubwa ya maendeleo." amesema Masele.
Aidha, amesema Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29 ulifanyika kwa Uhuru, Amani na haki, na viongozi sahihi wamepatikana, na kwamba kwa sasa ni kuwaunga mkono viongozi hao ili wawaletee maendeleo, huku akiwashaghaa wanaosema Uchaguzi huo haukuwa huru na haki.
TAZAMA PICHA👇👇
Katibu wa Siasa na Uenezi CCM Mkoa wa Shinyanga Richard Masele akizungumza kwenye Mkutano huo.
Katibu wa Siasa na Uenezi CCM Mkoa wa Shinyanga Richard Masele akizungumza kwenye Mkutano huo.
Katibu wa Siasa na Uenezi CCM Mkoa wa Shinyanga Richard Masele akizungumza kwenye Mkutano huo.
Diwani wa Puni Jumanne Rajabu akizungumza na wananchi wa Nyanshimbi kwenye Mkutano wa hadhara wa kuwashukuru kwa kumchagua kuwa Diwani wao.

Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464