` MWENYEKITI WA MISA TANZANIA EDWIN SOKO AWATAKIA WAANDISHI WA HABARI WOTE HERI YA NOEL

MWENYEKITI WA MISA TANZANIA EDWIN SOKO AWATAKIA WAANDISHI WA HABARI WOTE HERI YA NOEL


Edwin Soko awatakia waandishi wote heri ya Noel
xxx

Mwenyekiti wa MISA Tan na Mwandishi mwandamizi Edwin Soko amewatakia wanachama wa MISA Tan na Waandishi wote wa Tanzania heri ya sikukuu ya Noel.

Soko amesema anawatakia waandishi wote pamoja na familia zao *Heri ya Sikukuu ya Noeli,* iliyojaa amani, upendo na baraka tele.

'Tuitumie sikukuu hii takatifu kutafakari upya juu ya *upendo wa Mungu na kuimarisha upendo, mshikamano na umoja ndani ya tasnia yetu ya habari Tanzania" Alisema Soko

Soko ameongeza kuwa Na iwe ni wakati wa kujipatia nguvu mpya na msukumo wa kutekeleza kikamilifu majukumu yetu ya kikatiba katika kutafuta, kuchakata na kusambaza taarifa, huku tukiendelea kulinda na kutetea uhuru wa habari, uhuru wa kujieleza na haki ya wananchi kupata taarifa.

Aidha, amesema kuwa, waandishi wa habari waemdelew kuwa, mabalozi wa *haki, amani na maadili mema,* wachangia kwa vitendo kulinda na kudumisha ustawi wa Taifa letu.

Soko amehitimisha kwa kuaema anawatakia waandishi wote wa Tanzania heri ya sikukuu ya Noel na familia zao.
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464