` RC MHITA ATOA SALAMU ZA SIKUKUU YA KRISMASI NA MWAKA MPYA,MKOA UPO SHWARI KIUSALAMA

RC MHITA ATOA SALAMU ZA SIKUKUU YA KRISMASI NA MWAKA MPYA,MKOA UPO SHWARI KIUSALAMA

Na Marco Maduhu, SHINYANGA

MKUU wa Mkoa wa Shinyanga Mboni Mhita, ametoa salama za Sikukuu ya Krismasi na Mwaka mpya 2026, kwa wananchi wa Mkoa huo, huku akiwahakikishia kuwa mkoa upo shwari kiusalama.

Ametoa salama hizo leo Desemba 24,2025 wakati akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake.
RC Mboni Mhita.

“kwa heshima na unyenyekevu mkubwa, nawatakia wananchi wa Mkoa wa Shinyanga Kheri ya Krismasi na Mwaka mpya 2026,”amesema Mhita.

Amesema, mkoa huo upo shwari kiusalama na amani imeendelea kutawala, na wananchi wanaendelea na shughuli zao za kiuchumi kama kawaida, na kwamba washerehekee siku kuu hizo za mwisho wa mwaka kwa furaha na familia zao, huku akitoa tahadhari kwa madereva wa vyombo vya moto, wasiendeshe wakiwa wamelewa ili kuepusha ajali.

Amewaomba pia wananchi, wanapo sherehekea sikukuu hizo, wawakumbuke na watu wenye uhitaji, kwa kuwapatia misaada mbalimbali pamoja na kula nao chakula cha pamoja, ili nao wafurahie.

Aidha, amewataka wafanyabiashara mkoani humo wawe wazalendo na kuacha kupandisha bei za bidhaa, wakati wa msimu huu wa sikukuu, ili wananchi wa hali zote wapate kumudu kununua chakula na kufurahia na familia zao.

Amewashukuru pia wananchi, kwa kuendelea kushirikiana na Serikali, ikiwamo kulinda Amani, Rasilimali na kuwa Mabalozi wazuri wa Mkoa, na kwamba mwaka mpya 2026 uwe wa mafanikio kwa wananchi wote wa mkoa huo.
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464