Na Marco Maduhu, SHINYANGA
MKUU wa Mkoa wa Shinyanga Mboni Mhita, amewataka madiwani wa Manispaa ya Shinyanga kutanguliza maslahi ya wananchi mbele katika utekelezaji wa majukumu yao.
Amebainisha hayo leo Desemba 16,2025 wakati akizungumza kwenye kikao na Madiwani wa Manispaa hiyo, kilichofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa halmashauri.
Amesema, wananchi wanawaamini Madiwani hao, na ndiyo maana wakawapigia kura nyingi za ushindi Oktoba 29, pamoja na Mbunge Patrobas Katambi na Rais Dk.Samia Suluhu Hassan, kwamba wakati wa utekelezaji wa majukumu yao watangulize maslahi ya wananchi mbele.
“Nyie Madiwani ni daraja la kujenga mahusiano mazuri kati ya wananchi na serikali yao chini ya Rais Samia Suluhu Hassan, hivyo kumbukeni kutanguliza maslahi ya wananchi mbele, pamoja na kusikiliza na kutatua kero mbalimbali ambazo zinawakabili,”amesema Mhita.
Ameongeza”fanyeni mikutano na wananchi, tuleteeni yale ambayo wananchi wanayahitaji ili kutatua kero zao, fedha zipo za kutosha Serikali ya Rais Samia haijawahi kukaukiwa na fedha za utekelezwaji wa miradi ya maendeleo.”
Aidha, ameitaka Menejiment ya Manispaa hiyo kuziba mianya ya upotevu wa mapato pamoja na kuongeza ukusanyaji wa mapato na kubuni vyanzo vipya, na kwamba mapato ndiyo injini ya Halmashauri katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo na ongezeko la utoaji wa mikopo ya asilimia 10.
Pamoja na mambo mengine, Mkuu huyo wa Mkoa amewatakiwa Madiwani hao utekelezaji wao wa majukumu yao pamoja na kumtanguliza Mungu.
Kwa upande wake, Naibu Meya wa Manispaa ya Shinyanga, Pendo Sawa, akitoa neno la shukrani kwa niaba ya madiwani na Menejimenti ya Halmashauri, alimshukuru Mkuu wa Mkoa kwa nasaha na maelekezo aliyoyatoa.
Aliahidi kuwa madiwani na Menejimenti watazingatia maelekezo hayo kwa vitendo na kusimamia vyema utekelezaji wa miradi ya maendeleo kwa maslahi ya wananchi.
TAZAMA PICHA👇👇
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mboni Mhita akizungumza na Madiwani.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mboni Mhita akizungumza na Madiwani.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mboni Mhita akizungumza na Madiwani.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mboni Mhita akizungumza na Madiwani.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Julius Mtatiro akizungumza kwenye kikao cha Madiwani.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Julius Mtatiro akizungumza kwenye kikao cha Madiwani.
Naibu Meya wa Manispaa ya Shinyanga Pendo Sawa akizungumza kwenye kikao hicho.
Naibu Meya wa Manispaa ya Shinyanga Pendo Sawa akizungumza kwenye kikao hicho.
Naibu Meya wa Manispaa ya Shinyanga Pendo Sawa akizungumza kwenye kikao hicho.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mboni Mhita (kushoto)akiteta Jambo na Naibu Meya wa Manispaa ya Shinyanga Pendo Sawa.
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464