` MTENDAJI WA MAHAKAMA KUU BAKARI ALLY ATOA UJUMBE MZITO KWA WAZAZI:MAFAHALI YA 5 SHULE YA SEKONDARI LITLLE TREASURE

MTENDAJI WA MAHAKAMA KUU BAKARI ALLY ATOA UJUMBE MZITO KWA WAZAZI:MAFAHALI YA 5 SHULE YA SEKONDARI LITLLE TREASURE


Na Marco Maduhu, SHINYANGA

MTENDAJI wa Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Shinyanga Bakari Ally, amewataka wazazi kubadili mtindo wa maisha na kuacha kuendekeza masuala ya starehe bali wawekeze watoto wao kwenye elimu.

Ametoa Rai hiyo jana kwenye Mahafali ya Tano ya Shule ya Sekondari Little Treasure.
Amesema, wazazi wanapaswa kubadili mtindo wa maisha na kuacha kuendekeza masuala ya starehe kwa kufanya sherehe za ubatizo sh.milioni 3 au kufanya sherehe ya kuzaliwa na kutumia Laki 8 na linapofika suala la kulipia Ada Mtoto,wanaomba wavumiliwe.

“Wazazi wekeni vipaumbele vyenu kwenye mambo muhimu na kuacha kupoteza pesa hovyo, sasa hivi mwezi Desemba lakini unakuta mtu anafanya sherehe ya ubatizo anatumia hadi sh.milioni 3, au sherehe ya kuzaliwa sh.laki 8, ikifika januari unadaiwa Ada ya mtoto unasema huna hela,hivi unadhani Walimu watakuelewa kweli,”anasema Bakari.
“Maji ukiyavulia nguo lazima uyaoge, lipeni Ada kwa wakati, ukweli mchungu, lakini wazazi badilini mtindo wa maisha, kusomesha mtoto ni kufanya uwekezaji,”ameongeza.

Ametoa wito pia kwa shule ya Little Treasure, kuanzisha Club ya Sheria ambapo wanasheria kutoka Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Shinyanga watakuwa wakija kutoa elimu ya sheria shuleni hapo, na kuwajegea uelewa wa sheria.
Aidha, ametoa wito kwa wahitimu kuendelea kudumisha nidhamu kwa watu wote na kuwa mabalozi wazuri huo waendapo kwa kuitangaza vizuri shule yao.

Meneja wa shule hiyo Wilfred Mwita,amesema shule hiyo itaendelea kujituma kufundisha wanafunzi kwa juhudi zote na kufanya vizuri kitaaluma ili waziishi ndoto zao, huku akiomba ushirikiano kwa wazazi uendelee kuwa karibu na shule.
Mkurugenzi wa Shule za Msingi na Sekondari Little Treasure Lucy Mwita, amesema shule hizo zitaendelea kuwa hazina za watoto na daraja la mafanikio, na hata kutimiza ndoto zao, huku akitoa wito kwa wazazi waendelee kupeleka watoto wao shuleni hapo.

Naye Mkuu wa shule ya Sekondari Little Treasure Alfred Mathias, akisoma risala kwenye mahafali hayo, amesema jumla ya wanafunzi 61 wamehitimu, wavulana wakiwa 36 na wasichana 25.

TAZAMA PICHA👇👇
Mtendaji wa Mahakama kuu ya Tanzania Kanda ya Shinyanga Bakari Ally akizungumza.
Mkurugenzi wa Shule za Msingi na Sekondari Little Treasure Lucy akizungumza.
Meneja wa shule za Little Treasure Wilfred Mwita.
Mkuu wa shule ya Sekondari Little Treasure Alfred Mathias akisoma Risala ya shule.
Mwakilishi wa wazazi aliyekuwa Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko akizungumza.
Aliyekuwa Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko, akimpongeza mtoto wake Cedric kwa kuhitimu kidato cha Nne shule ya Sekondari Little Treasure.
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464