` AMANI: MSINGI MKUU WA KULETA MAPINDUZI YA TEKNOLOJIA KWA AJIRA ZA VIJANA

AMANI: MSINGI MKUU WA KULETA MAPINDUZI YA TEKNOLOJIA KWA AJIRA ZA VIJANA

Amani na utulivu wa nchi ni msingi mkuu unaowezesha mafanikio ya jitihada zote za Serikali, ikiwemo uwekezaji mkubwa unaofanywa katika sekta ya Elimu, Sayansi na Teknolojia. 

Bila amani, mageuzi yanayolenga kuwapa vijana ujuzi wa kitaalamu na wa kidijitali hayawezi kushamiri na kuleta tija katika soko la ajira.

Hii ndio sababu amani ni nguzo kuu kwa Teknolojia kushamiri na kuwanufaisha vijana:

Miundombinu ya Kitaaluma

Uwekezaji mkubwa unaofanywa na Serikali, ikiwemo ujenzi wa vyuo vya ufundi na mafunzo ya ufundi stadi (Polytechnics) katika mikoa mbalimbali, unahitaji mazingira salama ili ijengwe, iendeshwe, na itumike kwa ufanisi.

Matumizi ya TEHAMA: 

Amani inahakikisha shule, vyuo, na miundombinu ya TEHAMA (Teknolojia ya Habari na Mawasiliano) haiwezi kuvurugwa au kuharibiwa kutokana na machafuko, hivyo kuruhusu vijana kupata ujuzi wa Digital Literacy na Critical Thinking kwa uendelevu.

 Uwekezaji wa Nje (Diaspora na Washirika)

Serikali imeanzisha mikakati ya kuongeza mchango wa Watanzania wanaoishi nje (Diaspora) katika kutoa utaalamu, mbinu za kisasa za ufundishaji, na kuongeza fursa za ushirikiano na taasisi za ndani, amani ndio itawezesha hilo.

Itambulike kuwa wachangiaji wa nje (wataalamu, wawekezaji, na Diaspora) wanavutiwa kuleta maarifa, ubunifu, na mitaji yao tu katika nchi yenye amani, ambapo wanajua uwekezaji wao utakuwa salama na utaweza kuzaa matunda.

Akili unde (AI): 

Amani huwezesha ushirikiano katika maeneo magumu kama Akili unde (AI), kusaidia kuandaa vijana kwa ajira katika uchumi wa kidijitali.

Ushirikiano Kati ya Vyuo na Viwanda

Moja ya malengo ya Serikali ni kukuza ushirikiano kati ya vyuo vya elimu ya kati/juu na sekta ya viwanda, ili kuhakikisha wahitimu wanapata ujuzi unaohitajika sokoni.

Kiukweli amali na ujuzi wa kiteknolojia unaohitajika katika sekta ya fedha, simu na serikali unahitaji kuwepo kwa viwanda na makampuni yanayofanya kazi kwa utulivu na kuaminiana. Amani hutengeneza mazingira ya biashara na uzalishaji, ambapo vijana wanaweza kuajiriwa au kujiajiri (kwa kuanzisha kampuni zao).

Dira 2050: 

Waziri Mkenda amesema mipango inalenga kujenga rasilimali watu bora, nguzo muhimu ya kufikia malengo ya DIRA 2050. Amani ni chachu muhimu katika kufikia dira hiyo.

Kwa ufupi, amani ndiyo jukwaa ambalo juu yake uvumbuzi, uwekezaji, na mafunzo ya ujuzi wa kidijitali yanaweza kusimama, na hivyo kumuandaa kijana wa Kitanzania kuwa rasilimali watu yenye uwezo wa kushindana kimataifa. 

 

Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464