` SAUTI YA WANANCHI:MAOMBI,USHAURI NA SHUKRANI ZA WAATHIRIKA WA MACHAFUKO

SAUTI YA WANANCHI:MAOMBI,USHAURI NA SHUKRANI ZA WAATHIRIKA WA MACHAFUKO

 


Sauti za wananchi walioathirika katika vurugu  zilizoibuka hivi karibuni,zimeibua masuala muhimu yanayohitaji utatuzi, ikiwemo maombi ya msaada, ushauri kwa vijana, na pongezi kwa juhudi za Serikali.


Waathirika wakizungumza nafasi ya Serikali katika kupoinya majeraha yao wameiomba kuwaangaliwa waathirika wa moja kwa moja na uharibifu uliofanyika. 


Mama Everina Mosses Mmari, ambaye duka lake na mtaji wake wote viliungua, anaomba msaada wa Serikali kumwezesha kurejea kwenye biashara. Aidha Benjamin, mfanyabiashara, anashauri mamlaka husika kuendelea kuimarisha ulinzi katika jamii, akisisitiza kwamba vurugu hutumiwa kama fursa ya kupora na kuharibu. 


Hata hivyo, kuna pongezi kwa vikosi vya ulinzi, huku Shaban Moshi Shaban akipongeza jitihada zao za kurejesha utulivu na kuondoa changamoto.


Kwa upande wa ushauri kwa jamii na vijana, kuna msisitizo wa kupunguza jazba na kutafuta njia sahihi za kuwasilisha maoni. 


Gaspar Apolnary anashauri: "Sisi wenyewe tupunguze jazba, tufikishe maoni yetu. Wao wanatupa mawaidha na sisi tutoe maoni kwa namna nyingine ila kwa kufanya fujo inakuwa sio nzuri sana." 


Anabainisha kuwa fujo huathiri hata wale wasiohusika, mfano wagonjwa wanaoshindwa kupelekwa hospitali. 


Mama Everina naye alisisitiza haja ya wazazi kukaa na watoto wao na kuwashauri maisha yanaendaje. Kwa ujumla, ujumbe wa wananchi ni kwamba Tanzania imezoea amani na utatuzi wa changamoto za kitaifa ni jukumu la wote kwa utulivu.


Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464