` TUSIDHARAU SABABU ZA DOLA KULINDA MIUNDOMBINU

TUSIDHARAU SABABU ZA DOLA KULINDA MIUNDOMBINU

 

Katika mjadala wa matumizi ya nguvu ya vyombo vya dola, wachambuzi wa masuala ya usalama na utaratibu wameeleza kuwa kuna ugumu wa kiutendaji ambao hupingwa na taasisi za kidini, ambazo huzingatia zaidi haki kuliko wajibu wa Serikali kulinda miundombinu ya umma, ile ya hatari na mali za watu.

Biblia inatambua Mamlaka halali ya Serikali ya kutumia nguvu (upanga) ili kulinda raia na utaratibu dhidi ya uovu, kama ilivyoelezwa katika Warumi 13.

Katika maandiko hayo matakatifu Wajibu wa Dola umeelezwa kwa ufasaha zaidi: “Warumi 13:4: Maana yeye [mtawala/dola] ni mtumishi wa Mungu kwa ajili ya mema yako. Lakini ukifanya mabaya, ogopa; kwa maana haulichukui upanga bure.”

Pamoja na ukweli huo wa matumizi ya silaha za moto, watu wanaohoji walipaswa pia kuacha kupuuza ugumu wa vyombo vya usalama kudhibiti umati ulio na silaha au ulio na nia ya kufanya uharibifu wa miundombinu yenye hatari kubwa.

Mchambuzi mmoja wa masuala ya jamii alisisitiza kuwa kulenga tu kwenye Haki ya Kuishi na kuacha hatari kubwa inayowakabili wananchi kutokana na fujo za uharibifu sio sahihi.

"Pia kulikuwa na shaka nini kitatokea kama matangi hayo makubwa ya mafuta yatalipuka. Umbali wake ni kipenyo cha kilometa mbili."

Hii inabainisha kuwa matamshi yanayotaka haki yanapaswa kutambua wajibu wa Dola wa kulinda mali za raia na miundombinu muhimu ya Taifa, si tu dhidi ya waandamanaji bali pia dhidi ya majanga yanayoweza kutokana na uharibifu.

katika  mafundisho ya Biblia yanatambua kuwa Serikali ina jukumu la kuwadhibiti "watenda mabaya" ndani ya umati wa waandamanaji (1 Petro 2:13-14).

Mchambuzi huyo alisisitiza kuwa ingawa watu wanahaki ya kusema wanavyofikiri vitendo vya uharibifu vikubwa vinaweza kufanya hali hiyo ionekane tishio na hivyo vyombvo vya usalama kuchukua hatua amnbazo zinaweza kuumiza wengine.

Kutokana na uchambuzi wake amewataka Watanzania kuepuka kutumiwa na makundi yanayoona haki yao ya kuandamana ni muhimu zaidi kuliko usalama wa mali na utulivu wa taifa.

Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464