` TAASISI ZA DINI ZIMEKUMBUSHWA KUSIMAMIA UMOJA, SIYO UCHOCHEZI

TAASISI ZA DINI ZIMEKUMBUSHWA KUSIMAMIA UMOJA, SIYO UCHOCHEZI


 Kumekuwa na mjadala mkali unaoibua maswali kuhusu mwelekeo wa baadhi ya taasisi kubwa za kidini nchini, huku zikionekana kutumia ushawishi wao katika masuala yanayohusu miradi ya kitaifa na siasa.

Taasisi moja kubwa ya kidini nchini , imejikuta kwenye kikaango cha ukosoaji mkubwa, ikidaiwa kuwa sauti yake katika masuala ya kitaifa inaongozwa zaidi na "maslahi ya siri" badala ya maslahi mapana ya wananchi.

Sauti ya Nani? Taifa au Bahasha?

Baadhi ya wachambuzi wameonyesha wasiwasi wao kuhusu ukaribu uliopo kati ya baadhi ya viongozi wa taasisi hii na wanasiasa wa upinzani wenye nia ovu na taifa hili wakiwa na lengo la kuliparaganyisha tangu awali kwa kauli zao zinaohitimisha vurugu zilizofanyika Oktoba 29. Ukaribu huu unaibua maswali makuu mengi .

Swali la kwanza ni Je, kuna maslahi ya kisiasa yanayofichwa nyuma ya madhabahu? Pia ni kwa nini taasisi hii ilikaa kimya wakati wa matukio ya uchochezi, uasi, na uvunjifu wa amani, lakini sasa inahimiza "haki" ?Je, taasisi hii inatetea utulivu wa taifa au inalinda maslahi ya wachache?

Ukosoaji unazidi kusema kuwa taasisi hiyo inaonekana kutumia sauti ya imani kama njia ya kuweka presha, vitisho, na shinikizo (blackmail) kwa Serikali katika miradi ya kitaifa.

"Kila wimbi la kupinga, kila kelele ya lawama, linaonekana kuishia kwenye kitu kimoja: Bahasha, dili, na maslahi binafsi. Wanataka ionekane 'ni haki ya wananchi,' kumbe ni geuza mchezo wa kiroho kuwa biashara ya kivuli," inasema sehemu ya  mjadala huo.

Aidha mjadala huo katika mtandao unaonesha kwamba ili kuwepo na haki ni lazima kuwepo na mazingira ya amani kwani ni katika amani watu wanaweza kuzungumzia haki na kuona wapi iboreshwe.

"Marekani pamoja na kuwa na miaka 300 ya inayoitwa demokrasi bado kila kukicha watu wanajadili haki na kuona namna bora ya kutekeleza haki hizo ikiwa zina manufaa na ustawi wa jamii.Wanaweza kwa kuwa kumetengenezwa mazingira ya amani, kama hakuna hakuwezi kuwapo na majadiliano kama ilivyo Sudan kwa sasa"

Kumekuwa na madai yasiyothibitishwa yanayohusisha kelele hizo na kukatwa kwa mianya ya "uwizi pale bandarini" na Serikali ya sasa, jambo linaloaminika kuwa ndiyo chanzo cha malalamiko hayo.

Wazalendo wanasisitiza kwamba Amani haiuzwi, na taasisi za kidini hazipaswi kutumika kama kifaa cha kulazimisha maslahi ya wachache kwa njia ya presha ya kitaifa.

"Tanzania haitoe rushwa ya propaganda. Taifa linatoa ukweli," inahitimisha mijadala hiyo


Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464