
Kufuatia matukio ya hivi karibuni ya uchafuzi wa amani na uharibifu wa mali zikiwemo za watu binafsi Wilaya ya Bunda, Mkoa wa Mara, Watanzania wameungana na kutoa wito wa kitaifa wa kurejea kwenye hekima, upendo na umoja, huku wakikataa vikali vitendo vya vurugu.
Wakati uharibifu ukiendelea kuleta huzuni (kama inavyothibitishwa na ujumbe wa majonzi mtandaoni), dhamira ya umoja na maridhiano haijavunjika.
Wananchi walieleza hofu kubwa juu ya athari za vurugu, huku mmoja wa waathirika akisema kwa masikitiko, "Duka langu lilikuwa karibu na ofisi ya CCM daah." Kauli hizi zinathibitisha kuwa uharibifu hauathiri tu taasisi za umma bali pia wananchi binafsi.
Mchambuzi mmoja wa masuala ya kijamii alisisitiza: "Hakuna haki inayopatikana kwa vurugu na kutia hasara mali za watu binafsi, tulumbane kwa hoja zenye msingi za kuleta maendeleo kwenye nchi yetu na sio ugomvi." Hii inathibitisha kuwa amani ndio kitu muhimu aisee na ndio urithi wetu mkubwa.
Ulinzi wa Miundombinu na Urithi wa Nyerere
Taarifa kutoka kwa makundi mbalimbali zimesisitiza kwamba uharibifu wa mali na miundombinu vinakwamisha maendeleo ya nchi yetu.
"Vurugu zimeleta hasara kubwa sana kwa hiyo tuipende nchi kwa kudumisha amani na maendeleo yaweze kuja sasa," ilisema taarifa moja, ikisisitiza umuhimu wa kufuata sheria ili kuepuka hasara za mali na maisha. Maswali kuhusu "Utu wetu uko wapi" pia yaliibuliwa.
Akikumbusha msimamo wa kitaifa, kauli ya Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, ilitolewa tena kama onyo kwa wahujumu amani:
"Ukiona mtu anataka kuharibu amani ujue anahujumu uhuru wetu. Tusikubali kutumiwa kuvuruga tulichokijenga kwa miaka mingi."
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464