` AMANI NDIYO MTAJI:FAMILIA ZALIA NA MADENI KUFUATIA TAHARUKI

AMANI NDIYO MTAJI:FAMILIA ZALIA NA MADENI KUFUATIA TAHARUKI

Hasara kubwa ya kiuchumi imeripotiwa kufuatia vurugu, huku wananchi wa hali ya chini wakikosa hata riziki ya siku na kuingia kwenye madeni, jambo linaloonesha wazi umuhimu wa amani kama msingi wa maisha. Kipindi cha Lockdown kimeacha maumivu ya muda mrefu.

kijana mmoja ambaye hakupoenda kutaja jina lake anaeleza athari za moja kwa moja za kukosekana kwa amani na maandalizi hafifu ya kukabiliana na majanga ambayo yanatokea kwa kushtukiza.


"Ile lockdown imetusababishia madeni manake hatukuwa na chochote, kwanza tulikuwa hatuitarajii kutokea yale yaliyotokea. Pili, tunakuwaga hatuna akiba familia zetu nyingi. Wengine ndio tumetoka jana; sio siku tano, wengine tuna siku sita na wengine saba. Tudumishe amani, amani ndio kila kitu."


Faizat Peter, mkazi na mfanyabiashara wa Mbagala, anaeleza athari za kijamii na kiuchumi: "Kiufupi maandamano yalituathiri kiuchumi na kifamilia kiujumla. Maisha ya Mtanzania asilimia kubwa ni utoke ili upate kuishi. Watu wamepata taabu, familia zimeathirika, kulingana na kipato imekuwa taabu sana."


Mtaalamu wa Uchumi wa Familia  anasema, "Familia nyingi za Watanzania huishi kwa mapato ya siku. Kukaa ndani kwa siku tano hadi saba kunamaanisha wamepoteza mapato yote. Tunapaswa kujifunza kutokana na hili, tutaweza kudumisha utulivu wa kiuchumi kwa kuwa katika utaratibu, tusigeuze utaratibu" alisema.

 

Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464