` ITIKAFU YA KIISLAMU: MATUMIZI YA IBADA KATIKA KUSAKA SULUHISHO LA KITAIFA NA AMANI

ITIKAFU YA KIISLAMU: MATUMIZI YA IBADA KATIKA KUSAKA SULUHISHO LA KITAIFA NA AMANI


Tamko la Viongozi wa Taasisi za Kiislamu limeonesha namna ya kipekee ambavyo ibada na dini zinaweza kutumika kama suluhisho la changamoto za kitaifa. 

Viongozi hao waliamua kuingia kwenye Itikafu, ibada maalumu ya kujitenga na mengine yote ndani ya Msikiti, ili kujikurubisha kwa Mwenyezi Mungu, si tu kutoa dua, bali pia kutafakari njia sahihi ya kuivusha nchi.

Kama ilivyoelezwa katika tamko, Itikafu ilifanywa kufuata amri za Mungu za "Kimbilieni kwa Mola wenu" (Surat Addhaariyaat aya 50) na kutafuta ngazi ya kufikisha maombi kupitia ibada (Surah Al-Māʾidah: 35).

"Tumeona ni Muhimu kuwa na ibada hii ya itikafu baada ya matukio mazito yaliyoikumba nchi yetu siku ya uchaguzi mkuu..."

Hatua hii ya kiroho imesababisha maazimio thabiti yaliyolenga kurejesha amani, haki, na utulivu. Hii inasisitiza kwamba taasisi za Kiislamu zinatumia imani yao kama nguvu ya uongozi katika kipindi kigumu, huku wakiwaombea waliofariki na waliopata hasara, na kumsihi Mwenyezi Mungu awape nguvu na busara ya kukikabili kipindi hiki bila mpasuko.

Tamko hilo limehitimishwa kwa kuagiza Waislamu wote katika maeneo yao ya ibada (misikiti, madrasa, n.k.) kuendelea kumuomba Mwenyezi Mungu arejeshe na kudumisha amani iliyotetereka, kuashiria umuhimu wa jukumu la kila muumini katika ulinzi wa amani ya taifa.

Hali hiyo inatokana na ukweli kuwa japokuwa kampeni za Uchaguzi Mkuu wa 2025 zilifanyika kwa njia ya amani na utulivu,upigaji kura nao ulianza vizuri katika mikoa mingi ambapo wananchi walijitokeza  kupiga kura kwa amani, bila vurugu baadhi ya mikoa kulijitokeza fujo zilizolenga 

kuvuruga zoezi la kupiga na kuhesabu kura.   

Katika vurugu hizo nyumba na vituo vya mafuta vilichomwa, miundombinu ya umma iliharibiwa, biashara za watu binafsi zilivamiwa na kuchomwa moto, vituo vya polisi vilishambuliwa, ofisi kadhaa za Chama kimoja cha siasa zilichomwa moto, majengo ya Serikali Kuu na Serikali za Mitaa yalivamiwa na kuchomwa. Kubwa zaidi watu walijeruhiwa na kupoteza maisha, wakiwemo askari ambao walijitokeza kulinda mali na maisha ya raia. 

Taasisi za Kiislamu nchini Tanzania, pamoja na kulaani matukio haya na kusikitishwa sana na vifo vilivyotokea, upotevu wa mali za watu na 

uharibifu wa miundo mbinu uliotendeka na kuhuzunishwa na hali hiyo inahuzunishwa zaidi na kuwapo hadi sasa kwa makundi ambayo

yanatoa matamko ambayo kwa maudhui yake yanachochea na kuamsha hasira kwa namna ambayo yanahatarisha amani, utulivu, 

mshikamano na umoja wuliojengwa kwa miaka mingi tangu kuasisiwa kwa Taifa. 





Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464