Mtafiti na Mchambuzi kutoka TGNP, Wilfred Kulwa akizungumza kwenye mkutano wa mrejesho wa utafiti wa matokeo ya changamoto zinazotokana na athari za mabadiliko ya tabianchi uliofanywa na TGNP katika Kata ya Kiloleli, Wilayani Kishapu Mkoani Shinyanga Oktoba 13,2025
Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) umekamilisha utafiti wa awali kuhusu changamoto zinazotokana na athari za mabadiliko ya tabianchi katika Kata ya Kiloleli, Wilaya ya Kishapu Mkoani Shinyanga, ukiwa na lengo la kusaidia jamii kukabiliana na hali hiyo kwa njia endelevu.
Utafiti huo umehitimishwa Oktoba 13, 2025 kupitia mkutano wa mrejesho uliofanyika Kiloleli, ambapo wajumbe wa Kituo cha Taarifa na Maarifa wa Kata hiyo wamewasilisha matokeo yao kwa ubunifu kupitia maigizo, ngonjera na majadiliano ya kijiwe cha kahawa.
Kupitia njia hizo, washiriki wameonesha namna mabadiliko ya tabianchi yanavyoathiri shughuli za kila siku, ikiwemo upatikanaji wa maji,maisha ya kifamilia na mahudhurio ya wanafunzi shuleni.
Wananchi wametumia mkutano huo pia kutoa pongezi kwa serikali na wadau wa maendeleo(TGNP) kwa juhudi mbalimbali zinazofanyika katika kuboresha huduma muhimu kama maji, elimu na mikopo ya kiuchumi, huku wakihamasishwa kuendelea kushirikiana katika utekelezaji wa miradi hiyo.
Katika wasilisho hilo, washiriki wamesisitiza umuhimu wa kuendelea kuelimisha wanawake na vijana kuhusu fursa za mikopo yenye masharti nafuu inayotolewa na serikali, ili kuwawezesha kiuchumi na kupunguza utegemezi wa mikopo isiyo rasmi yenye masharti magumu"Kausha damu".
Afisa Maendeleo wa Kata ya Kiloleli, Mwigulu Donald, amesema serikali inaendelea kutoa elimu kuhusu mikopo ya serikali huku akiwataka wananchi kuendeleza ushirikiano na serikali katika kutatua changamoto zinazowakabili.
“Tunapaswa kuendelea kushirikiana katika kulinda watoto wetu, kufuatilia maendeleo yao shuleni na kujiandaa kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi kwa kutunza mazingira na kutafuta elimu itakayowasaidia kujikwamua kiuchumi Kwa kupata mbinu Mpya za kupata fedha” amesema Donald.
Kwa upande wake, Mtendaji wa Kata ya Kiloleli, Donald Mhangilwa, amesisitiza kuwa ushirikiano wa jamii na wadau ni nguzo muhimu ya maendeleo, akiwataka wananchi kuendelea kuunga mkono miradi ya serikali na ile inayoletwa na mashirika kama TGNP ambayo inalenga kuboresha maisha ya wananchi.
Mtafiti na Mchambuzi kutoka TGNP, Wilfred Kulwa, amemshukuru Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu, Emmanuel Johnson, kwa ushirikiano na utayari aliouonesha kuruhusu watafiti kufanya kazi hiyo muhimu.
Ameahidi kuwa TGNP itaendelea kushirikiana na serikali katika kutatua changamoto zinazotokana na mabadiliko ya tabianchi, hususani katika ngazi za jamii.
Mkutano huo umehudhuriwa na viongozi wa serikali ngazi ya kata na vijiji, walaghbishi, pamoja na wananchi wa Kata ya Kiloleli. TGNP yawapa hamasa wananchi wa Kiloleli kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi kupitia elimu, ubunifu na ushirikiano na serikali.
Mratibu wa Vituo vya Taarifa na Maarifa kutoka TGNP, Mwajuma Mkombozi akizungumza kwenye mkutano wa mrejesho wa utafiti wa matokeo ya changamoto zinazotokana na athari za mabadiliko ya tabianchi uliofanywa na TGNP katika Kata ya Kiloleli, Wilayani Kishapu Mkoani Shinyanga Oktoba 13,2025
Mwenyekiti wa Kijiji cha Kiloleli Iddy Luhende akizungumza kwenye mkutano wa mrejesho wa utafiti wa matokeo ya changamoto zinazotokana na athari za mabadiliko ya tabianchi uliofanywa na TGNP katika Kata ya Kiloleli, Wilayani Kishapu Mkoani Shinyanga Oktoba 13,2025
Mwenyekiti wa Kituo cha Taarifa na Maarifa Kata ya Kiloleli Kwangu Limbu akizungumza kwenye mkutano wa mrejesho wa utafiti wa matokeo ya changamoto zinazotokana na athari za mabadiliko ya tabianchi katika Kata ya Kiloleli, Wilayani Kishapu Mkoani Shinyanga Oktoba 13,2025
Mtendaji wa Kata Kiloleli Wilayani Kishapu Mkoani Shinyanga Donald Mhangilwa akizungumza kwenye mkutano wa mrejesho wa utafiti wa matokeo ya changamoto zinazotokana na athari za mabadiliko ya tabianchi katika Kata ya Kiloleli, Wilayani Kishapu Mkoani Shinyanga Oktoba 13,2025
Afisa Maendeleo ya Jamii Kata ya Kiloleli Wilayani Kishapu Mkoani Shinyanga Mwigulu Donald akizungumza kwenye mkutano wa mrejesho wa utafiti wa matokeo ya changamoto zinazotokana na athari za mabadiliko ya tabianchi uliofanywa na Shirika la TGNP katika Kata ya Kiloleli, Wilayani Kishapu Mkoani Shinyanga Oktoba 13,2025
Kupitia njia hizo, washiriki wameonesha namna mabadiliko ya tabianchi yanavyoathiri shughuli za kila siku, ikiwemo upatikanaji wa maji,maisha ya kifamilia na mahudhurio ya wanafunzi shuleni.
Wananchi wametumia mkutano huo pia kutoa pongezi kwa serikali na wadau wa maendeleo(TGNP) kwa juhudi mbalimbali zinazofanyika katika kuboresha huduma muhimu kama maji, elimu na mikopo ya kiuchumi, huku wakihamasishwa kuendelea kushirikiana katika utekelezaji wa miradi hiyo.
Katika wasilisho hilo, washiriki wamesisitiza umuhimu wa kuendelea kuelimisha wanawake na vijana kuhusu fursa za mikopo yenye masharti nafuu inayotolewa na serikali, ili kuwawezesha kiuchumi na kupunguza utegemezi wa mikopo isiyo rasmi yenye masharti magumu"Kausha damu".
Afisa Maendeleo wa Kata ya Kiloleli, Mwigulu Donald, amesema serikali inaendelea kutoa elimu kuhusu mikopo ya serikali huku akiwataka wananchi kuendeleza ushirikiano na serikali katika kutatua changamoto zinazowakabili.
“Tunapaswa kuendelea kushirikiana katika kulinda watoto wetu, kufuatilia maendeleo yao shuleni na kujiandaa kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi kwa kutunza mazingira na kutafuta elimu itakayowasaidia kujikwamua kiuchumi Kwa kupata mbinu Mpya za kupata fedha” amesema Donald.
Kwa upande wake, Mtendaji wa Kata ya Kiloleli, Donald Mhangilwa, amesisitiza kuwa ushirikiano wa jamii na wadau ni nguzo muhimu ya maendeleo, akiwataka wananchi kuendelea kuunga mkono miradi ya serikali na ile inayoletwa na mashirika kama TGNP ambayo inalenga kuboresha maisha ya wananchi.
Mtafiti na Mchambuzi kutoka TGNP, Wilfred Kulwa, amemshukuru Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu, Emmanuel Johnson, kwa ushirikiano na utayari aliouonesha kuruhusu watafiti kufanya kazi hiyo muhimu.
Ameahidi kuwa TGNP itaendelea kushirikiana na serikali katika kutatua changamoto zinazotokana na mabadiliko ya tabianchi, hususani katika ngazi za jamii.
Mkutano huo umehudhuriwa na viongozi wa serikali ngazi ya kata na vijiji, walaghbishi, pamoja na wananchi wa Kata ya Kiloleli. TGNP yawapa hamasa wananchi wa Kiloleli kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi kupitia elimu, ubunifu na ushirikiano na serikali.

Mwasilishaji wa matokeo ya changamoto zinazotokana na athari za mabadiliko ya tabianchi katika Kata ya Kiloleli, Wilayani Kishapu Mkoani Shinyanga kupitia njia ya maigizo baada ya utafiti uliofanywa na Shirika la Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) Oktoba 13,2025