` TAHADHARI KUTOKA KWA BWEGE: 'MAANDAMANO YANAWEZA KUWA MWISHO WA CHADEMA'

TAHADHARI KUTOKA KWA BWEGE: 'MAANDAMANO YANAWEZA KUWA MWISHO WA CHADEMA'

  

Aliyekuwa Mbunge wa Kilwa Kusini, Selaman Bungara, almaarufu "Bwege," ameibua mjadala mkali baada ya kutoa wito kwa Watanzania kujiepusha na maandamano yaliyopangwa kufanyika Oktoba 29.

Bungara ametahadharisha kuwa kushiriki katika hatua hiyo kutahatarisha amani ya nchi na huenda ikawa mwisho wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA).

Katika kauli yake, Bungara amewajibisha wananchi kutojihusisha na ghasia kwa kuwa amani ni kitu muhimu, huku akionyesha wasiwasi kuwa "hatujui chama gani kinaongoza, hatujui mtu anayeongoza" maandamano hayo.

Aidha amesema Oktoba 29 ni siku muhimu kwa taifa na wananchi wasikubali kuvuruga uchaguzi kwa sababu binafsi za watu wasiotakia mema nchi.

Kauli hii imepokelewa kwa hisia tofauti, hasa katika mitandao ya kijamii, huku baadhi ya wachangiaji wakimpongeza Bwege kwa "kuona mbele," wengine wakimkosoa vikali na kuhusisha msimamo wake na kubadili mwelekeo kisiasa.

Licha ya ukosoaji huo, jumbe za Bwege zimepata uungwaji mkono wanaoamini msimamo wake unalenga kulinda amani ya nchi.


Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464