Suzy Butondo,
Shinyangapressblog
SMAUJATA mkoa wa Shinyanga kwa kushirikiana na madaktari bingwa wa hospitali ya mkoa wa Shinyanga Mwawaza na Community Development initiaties wamezindua huduma ya kutoa elimu ya kupinga ukatili na kuhamasisha kutoa damu salama kwa ajili ya kuokoa maisha ya watu wakiwemo waliofanyiwa ukatili wa aina mbalimbali.
Huduma hiyo imezinduliwa leo katika manispaa ya Shinyanyanga kwa lengo la kutoa damu kwa hiari ili kupunguza vifo vya watu waliofanyiwa ukatili ikiwa ni pamoja na kutoa elimu ya kupinga ukatili wa aina yoyote.
Mwenyekiti wa SMAUJATA mkoa wa Shinyanga Nabila Kisendi akiambatana na mashujaa wote wakurugenzi na makatibu wa wilaya amesema zoezi hilo litakuwa endelevu,ambalo litafanyika kwa kila wilaya kwa ajili ya kuokoa maisha ya watu.
" Leo tumezindua katika manispaa ya Shinyanga lakini tutaendelea kutoa elimu hii katika wilaya zingine za mkoa wa Shinyanga, ambazo ni Kishapu, Kahama na Shinyanga vijijini,lengo letu sisi mashujaa wa maendeleo na ustawi wa jamii Tanzania mkoa wa Shinyanga ni kutoa elimu ya kupinga ukatili wa kijinsia na kutoa damu salama kwa hiari ili kupunguza vifo vya watu"amesema Kisendi.
"Niwashukuru mashujaa wote tulioambatana nao kwenye zoezi hili, Makamu mwenyekiti SMAUJATA mkoa Mwarabu Mhimbili,mwenyekiti wa manispaa Maryesther Nyarusanda, Husna Maige katibu manispaa, na viongozi wote wajumbe wote tulioambatana nao asanteni sana"amesema Kisendi.
Katibu wa wa SMAUJATA manispaa ya Shinyanga Hasna Maige amesema amesema mpaka sasa wamepima zaidi ya watu 80 waliotoa damu ni zaidi ya watu 20, hivyo watu wamejitokeza kwa wingi ambao wamepewa elimu ya kupinga ukatili wa kijinsia na wa aina yoyote.
Kwa upande wake Mratibu wa damu salama kutoka hospitali ya rufaa Mkoa wa Shinyanga Dkt Lissi Obed amesema zoezi hilo limefanyika vizuri, hivyo ameushukuru uongozi wa SMAUJATA kwa kuanzisha huduma hiyo ambayo ni ya kusaidia jamii.
"Naomba nichukue fursa ya kuwashukuru wananchi wote waliojitolea kutoa damu na niwashukuru SMAUJATA, kwani kitu walichokifanya ni kitu kikubwa, tumefanikiwa kupata chupa 12 za damu, hivyo tunahitaji ushirikiano wenu zaidi,"amesema Obedi.




















Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464