Kwa miaka mitano mfululizo, maisha yangu yalikuwa ya maumivu, machozi, na matumaini yaliyeyuka kila nilipoamka asubuhi. Nilikuwa nikihangaika na uvimbe tumboni uliokuwa unanisumbua sana, hasa wakati wa hedhi na nilipojaribu kufanya kazi za kawaida za nyumbani.
Nilipoteza uzito, nguvu, na hata imani yangu kwamba ningepona. Madaktari wengi walinambia suluhisho pekee lilikuwa upasuaji, jambo lililonitisha sana kwa sababu sikuwa na uwezo wa kifedha na pia niliogopa hatari zinazohusiana na upasuaji.
Familia yangu ilijaribu kila njia. Tulitembelea hospitali kadhaa na kutumia dawa za gharama kubwa, lakini hali yangu haikubadilika. Kila mwezi, maumivu yalizidi, na wakati mwingine nililala hospitalini kwa siku kadhaa bila matumaini.
Wengine walinambia labda nimekaliwa na mizimu au nimerogwa, wengine wakasema ni hali ya kawaida ya wanawake. Nilijikuta nimechanganyikiwa, nikishindwa kuelewa la kufanya.
Nilipoanza kuona damu ikitoka bila mpangilio na tumbo langu likianza kuvimba zaidi, nilijua lazima nifanye uamuzi. Nilikuwa nimechoka kuishi kwa maumivu na hofu. Nilianza kusali kila siku nikiomba muujiza, hata bila kujua ungekuja kutoka wapi. Nilikuwa na mtoto mchanga ambaye nilimzaa kwa shida, na hofu yangu kubwa ilikuwa kwamba ningeaga dunia kabla sijamlea.
