Baadhi ya wafanyabiashara wa Kata ya Masekelo Manispaa ya Shinyanga wakiwa kwenye mafunzo ya kuwajengea uwezo kuzitambua kodi wanazotakiwa kulipia pamoja na kueleza changamoto zinazowakabili ili zifanyiwe kazi.
Shirika lisilo la
kiserikali la Youth and Women Emancipation (YAWE) limewajengea uwezo
wafanyabiashara wa Kata ya Masekelo Manispaa
ya Shinyanga ili waweze kuelewa aina ya kodi ambazo huwa wanalipa
pamoja na kusikiliza kero zinazowakabili na kuweza kupatiwa ufumbuzi.
Hayo
yameelezwa na mwakilishi kutoka Shirika la YAWE Peter Nampala wakati wakitoa
mafunzo kwa wafanyabisha hao kupitia mradi wa kijana
wajibika ijue kodi yako lipa na shiriki inayosimamiwa na shirika la YAWE.
Amesema elimu iliyotolewa itawajenga wafanyabiashara na kuwawezesha kupata uelewa wa mambo ambayo yalikuwa ni kikwazo kwenye biashara zao,hatua ambayo itawainuwa kiuchumi na kuweza kulipa kodi zao kwa wakati.
Mwakilishi kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania TRA Mkoa wa Shinyanga kupitia dawati maalumu la uwezeshaji biashara Mkoji Wanjala akizungumza na wafanyabiashara Kata ya Masekelo.
“Leo tumekutana na wafanyabiashara
wa Kata ya Masekelo ambao wamepatiwa elimu juu ya kodi ya majengo,biashara na
namna ambavyo ushuru wa huduma unatakiwa kulipwa mambo ambayo wengi yalikuwa
yanawasumbua lakini baada ya elimu wamepata uelewa”amesema Nampela
Mwakilishi kutoka Mamlaka ya Mapato
Tanzania TRA Mkoa wa Shinyanga kupitia
dawati maalumu la uwezeshaji biashara Mkoji Wanjala amesema bado kuna tatizo la
uelewa wa kodi wanazotakiwa kulipia ikiwemo leseni ya biashara.
Amesema
uwepo wa dawati hilo litasaidia kuendelea kutoa elimu kwa wafanyabiashara juu
ya kodi mbalimbali ili kuwajengea uelewa zaidi ikiwa ni pamoja na kuzifanyia
kazi changamoto zilizopo ili kuweka mazingira mazuri kwa wate.



Mafunzo yanaendelea













Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464