Mr. Black akiwa na Balozi wa Tanzania nchini Rwanda, Mhe. Dkt. Habib Gallus Kambanga katika ubalozi wa Tanzania nchini Rwanda
Mr. Black akiingia katika Bunge Tukufu la Rwanda kwa shughuli maalumu
Kigali, Rwanda – 9 Oktoba 2025
Peter A. Frank Lugumi, anayejulikana pia kama Mr. Black, ambaye ni Mkurugenzi wa The BSL Investment Company Limited pamoja na BSL Schools Tanzania na Rwanda, na pia ni mjumbe wa Kamati ya Utekelezaji ya Jumuiya ya Wazazi kwenda Vijana (CCM Shinyanga Mjini), ameendelea na ziara yake ya kidiplomasia na uongozi nchini Rwanda.
Ziara hii inafuatia matembezi yake katika Ikulu ya Uganda tarehe 8 Oktoba 2025, ambapo leo Oktoba 9, 2025, amepata fursa ya kutembelea Bunge Tukufu la Rwanda kwa lengo la kuimarisha mahusiano na kuitangaza zaidi Tanzania kidiplomasia.
Katika hatua nyingine, Mr. Black amepokelewa rasmi katika Ubalozi wa Tanzania nchini Rwanda, ambako amekutana na Balozi wa Tanzania nchini Rwanda, Mhe. Dkt. Habib Gallus Kambanga, pamoja na Afisa Uwekezaji wa Ubalozi huo, Ndugu Mosses E. Mosses.
Mazungumzo yao yamejikita katika kuimarisha ushirikiano wa kiuchumi, elimu na uwekezaji kati ya Tanzania na Rwanda.
Vilevile, Mr. Black amepata nafasi ya kufanya mazungumzo na viongozi wa Bodi ya Uwekezaji ya Rwanda (RDB), hatua ambayo imezaa mafanikio kadhaa katika kukuza fursa za biashara na uwekezaji kwa nchi zote mbili.
Akiwa nchini Rwanda, Mr. Black ametembelea pia maeneo mbalimbali ya kihistoria kwa lengo la kukuza na kuendeleza historia ya Afrika Mashariki, pamoja na kuhamasisha utalii ndani ya Jumuiya ya Afrika Mashariki.
Kupitia muendelezo wa ziara hii, Mr. Black ameendelea kuwasisitiza vijana wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla kulinda amani, kuheshimu historia ya mataifa yetu, na kuendeleza mshikamano wa kikanda.
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464