` KAMPENI YA “KIJANA NA MAAMUZI KATIKA KUJENGA AMANI” YAENDELEA KUNG’ARA MTWARA

KAMPENI YA “KIJANA NA MAAMUZI KATIKA KUJENGA AMANI” YAENDELEA KUNG’ARA MTWARA

Mashirika matatu ya kijamii — ROTOSO, VOYOHEDE, na TASA — kwa kushirikiana na CEFA, yanaendelea kutekeleza kwa mafanikio kampeni ya “Kijana na Maamuzi katika Kujenga Amani” katika wilaya za Tandahimba, Mtwara Mjini, na Newala, mkoani Mtwara.

Kampeni hiyo, inayotekelezwa chini ya Mradi wa Kujenga Amani, inalenga kuhamasisha ushiriki wa vijana katika michakato ya maamuzi ili kupunguza migogoro na kuimarisha umoja katika jamii.

Kampeni hiyo inafanyika kwa kushirikiana moja kwa moja na vijana katika maskani na vijiweni, sambamba na vipindi vya redio vinavyosisitiza umuhimu wa sauti ya vijana katika ujenzi wa amani.

Aidha, kampeni inapania kubadilisha mitazamo hasi dhidi ya vijana, ikionyesha kuwa vijana ni nguvu muhimu ya mabadiliko chanya na maendeleo endelevu katika jamii.

Ujumbe mkuu wa kampeni unasema: “Kila uamuzi mdogo unajenga amani kubwa”,ukisisitiza kwamba kila kijana ana nafasi muhimu katika kujenga amani na ustawi wa taifa.

#PowerOfYouth
#JengaAmani
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464