` JUMUIYA YA WAZAZI KATA YA NGOKOLO YASAKA KURA MTAA KWA MTAA

JUMUIYA YA WAZAZI KATA YA NGOKOLO YASAKA KURA MTAA KWA MTAA

                         

             Suzy Butondo,Shinyanga

Jumuiya ya wazazi kata ya Ngokolo manispaa ya Shinyanga ikiongozwa na wajumbe wa kamati ya utekelezaji wazazi wilaya imefanya ziara ya kusaka kura za Chama Cha Mapunduzi mtaa kwa mitaa.

Zoezi hilo ambalo liliongozwa na mjumbe wa kamati ya utekelezaji Jumuiya ya wazazi wilaya Daniel Kapaya akiambatana na wajumbe wa kamati ta utekelezaji wazazi kata ya Ngokolo pamoja na mgombea udiwani kata ya Ngokolo Jackiline Isalo wametembelea mitaa kwa mitaa, kwa wauza kahawa,kwenye migahawa na wajasiliamali wa matunda na mboga mboga

Mjumbe wa kamati ya utekelezaji jumuiya ya wazazi wilaya Daniel Kapaya ambaye ndiye aliongoza jopo la kusaka kura hizo amewaomba wananchi wa kata ya Ngokolo wachague wagombea wa chama cha mapinduzi CCM kuanzia Rais,Katambi na diwani ili waweze kuendeleza kuleta maendeleo.

"Chama cha mapinduzi ni chama chenye ilani ya kuleta mabadiliko kwa wananchi wote, hivyo tunawaomba wanangokolo wote tuendelee kukiamini chama cha Mapinduzi ambacho kitasimamia maendeleo hivyo niwaombe mjitokeze wote tarehe 29 kwenda kupiga kura tupitie rafiki zetu na tutunze viparaya vyetu vizuri ili siku hiyo tunaenda kutiki tu"amesema Kapaya.

Kwa upande wake mgombea wa udiwani wa kata ya Ngokolo Jackiline Isalo amewaomba wananchi wa kata ya ngokolo wampe kura za kutosha ili aweze kuwaletea maendeleo kata ya Ngokolo, pia amewaomba wamchague mbunge Patrobas Katambi na Rais Samia Suluhu Hassan ambao atashirikiana nao katika kuleta mabadiliko katika kata ya Ngokolo na Taifa kwa ujumla.

"Wazazi wangu ndugu zangu nimepiga magoti kuwaomba kura zenu zote mkipigie chama cha mapinduzi ili kiweze kuwaletea maendeleo katika kata yetu ya Ngokolo, mkituchagua kwa kushirikiana na viongozi wenzangu tutaendeleza pale tulipoishia na kufanya maboresho zaidi ili kuhakikisha maisha ya kila mmoja yanaboreka kiuchumi,"amesema Jackiline.


























Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464