Na Sumai Salum - Kishapu
Mkuu wa Wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga, Mhe. Peter Masindi, amewataka wananchi wote wa Wilaya hiyo kushiriki kikamilifu katika zoezi la upigaji kura litakalofanyika Oktoba 29, 2025, ili kuchagua viongozi watakaosimamia vyema maendeleo na rasilimali za taifa.
Akizungumza leo Oktoba 25, 2025, baada ya kumaliza zoezi la jogging ya kilomita 7 lililofanyika katika maeneo mbalimbali ya Mji Mdogo wa Mhunze, Mhe. Masindi amewahimiza wananchi kutambua umuhimu wa kura kama nyenzo ya msingi ya kuleta mabadiliko chanya katika jamii.
Zoezi hilo la mazoezi lilianzia katika viwanja vya michezo vya Shule ya Msingi Buduhe na kumalizikia katika Soko la Swalala, lililopo katika Mtaa wa Mnada wa Zamani Kata ya Kishapu.
Katika hotuba yake, Mhe. Masindi amesisitiza umuhimu wa kudumisha amani na utulivu kipindi chote cha uchaguzi, kujiepusha na vitendo vya uchochezi na propaganda zisizo na msingi, pamoja na kuheshimu matokeo yatakayotangazwa na mamlaka husika.
“Kura yako ni haki yako. Ukiogopa kupiga kura, umeogopa kutengeneza taifa lako. Tuende tukashiriki kwa amani na upendo,” amesema Mhe. Masindi.
Katibu Tawala Wilayani Kishapu Mkoani Shinyanga Fatma H. Mohammed
Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu, Bw. Emmanuel Johnson, amewataka wananchi kufanya mazoezi mara kwa mara kwa ajili ya kulinda afya zao na kuongeza tija katika uzalishaji.
“Mazoezi ni chanzo cha afya bora. Afya njema huleta nguvu ya kufanya kazi na kuchangia maendeleo ya taifa. Tumeweka utaratibu wa kufanya mazoezi kama haya kila Jumamosi tukishirikiana na wananchi, watumishi wa serikali na taasisi zisizo za kiserikali,” ameeleza Bw. Johnson.
Zoezi hilo limehusisha wananchi wa kawaida, wanafunzi, watumishi wa umma, pamoja na wawakilishi wa taasisi mbalimbali, likiwa na lengo la kuhamasisha utamaduni wa mazoezi, mshikamano na ushiriki wa kijamii katika masuala ya maendeleo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu Mkoani Shinyanga Emmanuel Johnson 

Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464