` ASCO LOUNGE KUZINDUA MSIMU WA BURUDANI KWA MATENDO,BELLE 9 KUTUMBUIZA

ASCO LOUNGE KUZINDUA MSIMU WA BURUDANI KWA MATENDO,BELLE 9 KUTUMBUIZA

Na Marco Maduhu,SHINYANGA

ASCO Lounge ya mkoani Shinyanga inakwenda kuzindua msimu wa burudani kwa matendo, ikiwa ni jukwaa muhimu la kukuza burudani za nyumbani na kuibua vipaji vya vijana.

Mratibu wa maudhui yenye tija kutoka Asco Lounge, Yusuph Magupa, amebainisha hayo leo Oktoba 25, 2025, wakati akizungumza na waandishi wa habari.
Amesema Asco Lounge ni nyumba ya burudani yenye dhamira ya kushibisha radha ya starehe kupitia vinywaji, muziki na chakula bora, huku ikijikita kubeba sanaa, kusambaza muziki mzuri katika hafla, burudani za klabu na kujenga taasisi imara za burudani.

“Leo Oktoba 25, 2025 tunazindua ‘Action Season One’, yaani msimu wa burudani kwa matendo hapa Asco Lounge. Tutakuwa na onyesho maalumu kutoka kwa msanii mwenye ushawishi mkubwa katika uimbaji wa maudhui ya kijamii nchini Tanzania, ambaye si mwingine bali ni Belle 9,” amesema Magupa.
Ameongeza kuwa Asco Lounge inajitambulisha kama jukwaa muhimu la burudani za nyumbani linalochochea utamaduni wa mitaani, na wako tayari kuandaa maudhui kwa ajili ya televisheni, redio, televisheni mtandaoni na matamasha makubwa.

Magupa amesema pia wanakuja na mradi wa Talanta za Maskani, unaolenga kuonesha vipaji vya nyumbani kutoka kila kona ya Tanzania, kwa imani kuwa kila kanda ina hazina ya vipaji. Mradi huo utatumia kaulimbiu “Nguvu ya Kitaa Ikiwika – Kanda ya Ziwa Inaamka.”
Aidha, amesema kila Jumamosi kuanzia saa 4:00 asubuhi hadi saa 10:00 jioni kutakuwa na jukwaa la kuonesha vipaji vya muziki, uchekeshaji, maigizo na sanaa nyinginezo, ikiwa ni hatua ya awali ya kuunda maudhui yatakayobeba fahari ya vipaji vya maskani.

Kwa upande wake, msanii wa kizazi kipya Belle 9 ameipongeza Asco Lounge kwa kuzindua msimu huo wa burudani kwa matendo, akisema utakuwa chachu ya kutoa burudani kwa wakazi wa Shinyanga na kuchochea ukuaji wa vipaji vya vijana.

TAZAMA PICHA👇👇
Mratibu wa maudhui yenye tija kutoka Asco Lounge Yusuph Magupa akizungumza na waandishi wa habari.
Mratibu wa maudhui yenye tija kutoka Asco Lounge Yusuph Magupa akizungumza na waandishi wa habari.
Mratibu wa maudhui yenye tija kutoka Asco Lounge Yusuph Magupa akizungumza na waandishi wa habari.
Msaani wa kizazi kipya Belle 9 akizungumza na waandishi wa haabri.

Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464