Na Marco Maduhu,SHINYANGA
MGOMBEA Udiwani wa Chama cha Mapinduzi CCM Kata ya Ngokolo Jackile Isaro,ameendelea na kampeni zake katika Mtaa wa Kalonga,huku akiwahidi wananchi kwamba watajenga kituo cha Afya Kata ya Ngokolo ili wapate matibabu bora na sahihi.
Akizungumza leo Oktoba 20,2025 katika Mkutano huo,amesema yeye ahadi zake niza uhakika na siyo kutoa kichwani, sababu ahadi hizo zipo kwenye Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2025-2030.
Amewaomba wananchi waendelee kukiamini Chama cha Mapinduzi CCM,na kukipatia tena ridhaa ya kuendelea kuwa madarakani, ili kiendelee kuwaletea maendeleo ya kweli yanayotokana na ilani makini yenye kujali maslahi ya wananchi.
“Kata ya Ngokolo tunakwenda kujenga Kituo cha Afya na siyo Zahanati,hili lipo kwenye ilani ya CCM, na ilani yetu ni mkataba baina ya CCM na wananchi,hivyo endelee kukiamini Chama Cha Mapinduzi na siku ya Uchaguzi Mkuu Oktoba 29 kawapigieni kura wagombea wote wa CCM kuanzia Rais Samia,Mbunge Katambi na Madiwani nikiwamo mimi,”amesema Jackline.
Aidha,ametuma salamu kwa wapinzani ambao wamekuwa wakiendekeza kampeni za kumchafua, kuwa yeye hajafundishwa na Chama chake kufanya kampeni za namna hiyo, bali atawajibu kwa kutekeleza miradi ya maendeleo kwenye Kata.
TAZAMA PICHA👇👇
Mgombea Udiwani Kata ya Ngokolo kupitia CCM Jackline Isaro akinadi sera kwa wananchi pamoja na kuomba kura.





















































