Na Marco Maduhu,SHINYANGA
MGOMBEA Udiwani wa Kata ya Shinyanga Mjini kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM) Salum Kitumbo,ameendelea na mikutano yake ya kampeni kwa kunadi sera na ilani ya CCM kuelekea Uchaguzi Mkuu Oktoba 29,ili wananchi wamchague awe diwani wao,pamoja na kumpigia kura Mgombea Ubunge Jimbo la Shinyanga Patrobas Katambi,na kura za kishindo kwa Rais Dk.Samia Suluhu Hassan.
Leo Oktoba 6,2025 Kitumbo amefanya Mkutano wa kampeni pamoja na kusikiliza kero za wananchi wa Kata ya Shinyanga Mjini,na kuahidi kuzitatua endapo wakimpatia ridhaa ya kuwa Diwani wao katika Uchaguzi Mkuu Oktoba 29 mwaka huu.
Amesema,kero mbalimbali ambazo zimewasilishwa na wananchi, kwamba amezichukua na kama “assignment” kwake, na siku tu akiwa Diwani wa Kata hiyo, ataanza nazo kama kipaumbele chake, ili Kata ya hiyo ipige hatua kubwa ya kimaendeleo.
Aidha,akijibu kero ya kutokamilika kwa uzio wa Shule ya Msingi Town,amesema kwamba uzio huo ataukamilisha, lakini kabla ya ujenzi wake,ataangalia kwanza kama sheria inaruhusu ili wajenge Maduka kwa kuzunguka shule hiyo,ili wafanya biashara wapate sehemu ya kufanyabiashara,pia shule ipate mapato na kuongeza mapato ya Halmashauri na taifa kwa ujumla.
Amejibu pia swali la mikopo, kwamba akiashaingia Halmashauri itapiga pia suala hilo ili wanawake,vijana na watu wenye ulemavu wapate mikopo ya halmashauri asilimia 10 ambayo haina riba na kuinuka kiuchumi, kwa kuondokana na mikopo kausha damu.
“Kero zote ambazo mmeziwasilisha kwangu na waombeni siku ya Uchaguzi Oktoba 29 mjitokeze kwa wigi mkanipigie kura ili nipate kuwa diwani wenu,mpigieni pia Patrobas Katambi, na Rais wetu Dk.Samia Suluhu Hassan,ili tuchape kazi kwa ushirikiano,umoja na kuwaletea maendeleo,”amesema Kitumbo.
Ametoa ahadi nyingine,kwamba atahakikisha barabara zote za Kata ya Mjini zinawekwa Lami,Taa za Barabarani,kukamilisha ujenzi wa Soko Kuu la Shinyanga Mjini,pamoja na ajira zote ambazo zitakuwa zikitoka Halmashauri kipaumbele kitwakuwa kwa vijana wa Kata hiyo.
Mwenyekiti wa UVCCM wilaya ya Shinyanga Mjini Abdulaziz Sakala,akizungumza kwenye mkutano huo wa kampeni,amesema Kata ya Shinyanga Mjini imepata Diwani ambaye ni Mwadilifu,mchapakazi na anapenda kufanya mambo makubwa na kuwashidi siku ya Uchaguzi Oktoba 29 wasifanye makossa bali waka tiki tiki 3 kwa Kitumbo,Katambi na Rais Dk.Samia Suluhu Hassan.
Nao Madiwani wa Kata jirani na Vitimaalum,ambao walimuunga Mkono mwenzao,wamewaomba wananchi,kwamba waichague CCM, sababu ina sera na ilani inayotekelezeka na imegusa maslahi ya wananchi.
TAZAMA PICHA👇👇
Mgombea Udiwani Kata ya Shinyanga Mjini Salum Kitumbo akiwa kwenye mkutano wake wa kampeni.
Mgombea Udiwani wa Kata ya Shinyanga Mjini Salum Kitumbo akinadi sera na Ilani ya CCM kwa wananchi.
Mwenyekiti wa UVCCM wilaya ya Shinyanga Mjini Abdulaziz Sakala akizungumza kwenye mkutano wa kampeni
Diwani Mteule wa Vitimaalum MwanaKhamis Kazoba akiomba kura kwa wananchi.
Diwani Mteule wa Vitimaalum MwanaKhamis Kazoba akiomba kura kwa wananchi.
Diwani Mteule wa Vitimaalum MwanaKhamis Kazoba akisalimiana na Mgombea Udiwani wa Kata ya Shinyanga Mjini Salum Kitumbo mara baada ya kumaliza kumuombea kura kwa wananchi.
Diwani Mteule wa Vitimaalum Veronica Masawe akiomba kura kwa wananchi kumchagua Salum Kitumbo na wagombea wote wa CCM.
Mgombea Udiwani wa Ibinzamata Ezekiel Sabo akimwombea kura Kitumbo na wagombea wote wa CCM.
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464