` THBUB YATAHADHARISHA ATHARI ZA TAARIFA ZA UONGO KIPINDI CHA UCHAGUZI

THBUB YATAHADHARISHA ATHARI ZA TAARIFA ZA UONGO KIPINDI CHA UCHAGUZI

Kamishna wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB), Nyanda Shuli, akizungumza wakati akifungua mafunzo kwa waandishi wa habari Mkoa wa Shinyanga kuhusu haki na wajibu wao katika kipindi cha uchaguzi.

Na Kadama Malunde – Shinyanga

Waandishi wa habari mkoani Shinyanga wametakiwa kuzingatia weledi, maadili na kutokuegemea upande wowote wakati wa kuripoti masuala ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2025, ili kulinda amani na taswira chanya ya taifa ndani na nje ya mipaka yake.

Wito huo umetolewa leo Jumatano Septemba 24, 2025, na Kamishna wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB), Nyanda Shuli, wakati akifungua mafunzo kwa waandishi wa habari kuhusu haki na wajibu wao katika kipindi cha uchaguzi.

“Maadili ya uandishi wa habari tuyasimamie vizuri. Tumieni taarifa za kweli badala ya taarifa za kupika ili tuvuke salama kwenye uchaguzi. Tunataka kuiona Tanzania ya kabla ya uchaguzi, iwe hiyo hiyo wakati na baada ya uchaguzi. Nchi zingine zinaiona Tanzania kama mfano, hivyo tunatamani taswira hiyo ibaki,” amesema Shuli.

Amesisitiza waandishi wa habari kutokuwa mashabiki au makada wa vyama vya siasa, bali kuendelea kulinda taaluma yao kwa kuripoti habari sahihi, zenye usawa na kuzingatia maslahi ya taifa.

“Tusikubali kuwa maafisa uhusiano wa wanasiasa hata kama unawafahamu wagombea. Usikubali kutumika kama Big G, utamu ukiisha unatupwa. Habari zetu zionekane zimeandikwa na waandishi waliobobea,” ameongeza.

Kamishna wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB), Nyanda Shuli.

Aidha, Shuli amewahimiza waandishi kutumia kalamu zao kuelimisha wananchi kuhusu masuala ya uchaguzi, ikiwemo umuhimu wa kuhudhuria mikutano ya kampeni, kupata taarifa sahihi na kujitokeza kupiga kura Oktoba 29, 2025.

Akitoa mada kuhusu haki na wajibu wa waandishi wa habari kipindi cha uchaguzi, Afisa Mchunguzi Mkuu wa THBUB, Brighton Mwiga, amesema waandishi wa habari ni nguzo muhimu katika kulinda haki za binadamu na misingi ya utawala bora.

Amezitaja haki muhimu za wananchi wakati wa uchaguzi kuwa ni: haki ya kuchagua na kuchaguliwa, haki ya kupata taarifa, uhuru wa maoni, uhuru wa kukusanyika, kutokubaguliwa, haki ya kuishi na usalama wa mtu, pamoja na haki ya kupata nafuu kupitia vyombo vya sheria.
Afisa Mchunguzi Mkuu wa THBUB, Brighton Mwiga.

Kwa upande wa wajibu wa waandishi wa habari, Mwiga ameeleza kuwa waandishi wanapaswa kuelimisha wananchi kuhusu uchaguzi ili waweze kufanya maamuzi sahihi; kuripoti habari kwa usahihi na bila upendeleo; kuheshimu usiri wa wapiga kura; kuhamasisha wananchi wenye sifa kushiriki uchaguzi; kufichua vitendo vya uvunjaji wa haki za binadamu; na kuepuka kutumia lugha ya uchochezi, chuki au taarifa zinazoweza kuibua vurugu katika jamii.

Mwiga ameonya kuwa upotoshaji wa habari unaweza kusababisha madhara makubwa ikiwemo kuchanganya umma, kuvuruga maamuzi ya kisiasa, kuchochea migogoro, kupoteza imani ya wananchi kwa vyombo vya habari, kuchafua heshima ya watu au taasisi, na hata kuathiri uchumi wa taifa.
 “Ni ukweli usiopingika kuwa waandishi wa habari wana nafasi kubwa kwa jamii hasa kipindi cha uchaguzi. Kwa kupitia taaluma yenu mna uwezo wa kulinda haki za binadamu au kushiriki kwenye uvunjifu wa haki hizo. Ni wajibu wenu kuhakikisha wananchi wanapata fursa ya kutumia haki yao ya kikatiba kushiriki uchaguzi,” amesisitiza Mwiga. 

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoa wa Shinyanga (Shinyanga Press Club - SPC), Greyson Kakuru ameishukuru Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora kwa kuandaa mafunzo hayo muhimu, akibainisha kuwa yamekuja wakati muafaka kuelekea uchaguzi mkuu wa mwaka 2025.
 Mwenyekiti wa SPC Greyson Kakuru.

Amesema mafunzo hayo yatawasaidia waandishi wa habari kuongeza uelewa juu ya haki na wajibu wao, kuimarisha weledi katika kazi zao, na kuhakikisha wanachangia kulinda amani na mshikamano wa kitaifa. 

Kakuru ameahidi kuwa SPC itaendelea kushirikiana kwa karibu na wadau mbalimbali ili kuhakikisha waandishi wa habari wanatimiza majukumu yao kwa kuzingatia maadili na weledi wa taaluma.
Kamishna wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB), Nyanda Shuli, akizungumza wakati akifungua mafunzo kwa waandishi wa habari Mkoa wa Shinyanga kuhusu haki na wajibu wao katika kipindi cha uchaguzi.
Kamishna wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB), Nyanda Shuli, akizungumza wakati akifungua mafunzo kwa waandishi wa habari Mkoa wa Shinyanga kuhusu haki na wajibu wao katika kipindi cha uchaguzi.
Kamishna wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB), Nyanda Shuli, akizungumza wakati akifungua mafunzo kwa waandishi wa habari Mkoa wa Shinyanga kuhusu haki na wajibu wao katika kipindi cha uchaguzi.

Kamishna wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB), Nyanda Shuli, akizungumza wakati akifungua mafunzo kwa waandishi wa habari Mkoa wa Shinyanga kuhusu haki na wajibu wao katika kipindi cha uchaguzi.
Kamishna wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB), Nyanda Shuli, akizungumza wakati akifungua mafunzo kwa waandishi wa habari Mkoa wa Shinyanga kuhusu haki na wajibu wao katika kipindi cha uchaguzi.

Kamishna wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB), Nyanda Shuli, akizungumza wakati akifungua mafunzo kwa waandishi wa habari Mkoa wa Shinyanga kuhusu haki na wajibu wao katika kipindi cha uchaguzi.
 Mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoa wa Shinyanga (Shinyanga Press Club - SPC), Greyson Kakuru akizungumza wakati wa mafunzo yaliyotolewa na Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB) kwa waandishi wa habari Mkoa wa Shinyanga kuhusu haki na wajibu wao katika kipindi cha uchaguzi.
Afisa Mchunguzi Mkuu wa THBUB, Brighton Mwiga akitoa mada kuhusu haki na wajibu wa waandishi wa habari kipindi cha uchaguzi
Afisa Mchunguzi Mkuu wa THBUB, Brighton Mwiga akitoa mada kuhusu haki na wajibu wa waandishi wa habari kipindi cha uchaguzi
 Waandishi wa habari wakifuatilia mada kuhusu haki na wajibu wa waandishi wa habari kipindi cha uchaguzi

Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464