Mhifadhi Misitu wa Wilaya ya Kishapu Tumaini Masatu Mwijarubi akieleza hatua za serikali za kuondoa gharama za miche ili kila mwananchi awe sehemu ya uhifadhi wa mazingira Septemba 10,2025.
Baadhi ya Wananchi Wilayani Kishapu Mkoani Shinyanga wameipongeza Ofisi ya Wakala wa Huduma za Misitu (TFS) kwa ushirikishwaji wa karibu katika masuala ya Uhifadhi wa Misitu na mazingira Kwa kupata mafunzo ya uandaaji na upandaji miti, hatua inayowajengea uelewa na fursa mpya za kiuchumi.
Mbali na kuwa ni sehemu yao ya muda ya kujipatia kipato wametoa pongezi hizo Septemba 10, 2025 waliposhiriki katika zoezi la awali la utengenezaji viliba, ujazaji udongo na upangaji miche.
Wakazi wa Kitongoji cha Mhunze ya Juu, Kwandu Kusekelwa na Moshi Mahona wamesema elimu waliyopewa na TFS ni tofauti na ile waliyokuwa wakipata mitaani, kwani imejikita katika mbinu za kisayansi na endelevu za uhifadhi wa mazingira.
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464
Wakazi wa Kitongoji cha Mhunze ya Juu, Kwandu Kusekelwa na Moshi Mahona wamesema elimu waliyopewa na TFS ni tofauti na ile waliyokuwa wakipata mitaani, kwani imejikita katika mbinu za kisayansi na endelevu za uhifadhi wa mazingira.

Mwananchi wa Kitongoji cha Mhunze ya Juu, Moshi Mahona
“Tumepata elimu kubwa sana ya uandaaji na uoteshaji miche. Serikali inatoa mikopo ya 10% kupitia Halmashauri, na mara nyingi tunafikiria kuomba ili tuanzishe biashara ya uuzaji miche ila tunapata hofu kuomba fedha kwani tunapata hasara kutokana na Wananchi wengi kitokufahamu umuhimu wa kupanda miti, hivyo ni vyema elimu hii ikaendelea kutolewa,” amesema.
Ameongeza kuwa wamepata elimu ya jinsi ya kuandaa mashimo yatakayopelekea mmea kustawi na kukuwa na jinsi ya kuandaa mchanga,udongo na samadi kwenye mche tofauti na elimu za mitaani ambazo hazina utalamu kiasi Cha kupelekea miche kufa.
Kwa upande wake, Gidion Mathias, mwanafunzi wa kidato cha pili Wilayani humo amesema anatamani kuwa balozi wa mazingira kwa kujifunza zaidi namna ya kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi kupitia elimu anayoipata kutoka TFS kwa masaa ya ziada akiwaendea.
Akizungumzia mikakati ya taasisi hiyo, Mhifadhi Misitu wa Wilaya ya Kishapu, Tumaini Masatu Mwijarubi, amesema katika mwaka wa fedha 2025/2026 TFS Kishapu imelenga kuotesha miche 200,000 ya matunda, mbao na kivuli, ambayo itagawiwa bure kwa wananchi wakati wa msimu wa mvua utakapoanza.
“Serikali imeamua kusaidia wananchi kwa kuondoa vikwazo vya gharama za ununuzi wa miche. TFS tumekabidhiwa jukumu la kuotesha na kugawa miche hiyo bure, huku gharama zikibebwa na serikali. Lengo letu ni kuhakikisha kila mwananchi anashiriki katika kuhifadhi mazingira,” amesema Mwijarubi.
Aidha, amebainisha kuwa TFS itaendelea kushirikisha wananchi si tu kwa ajili ya upandaji miti, bali pia kuwajengea uwezo wa utunzaji misitu, ili kuongeza ushiriki wao katika mnyororo wa thamani wa zao la misitu.
Mwanafunzi wa kidato cha pili Gidion Mathias akieleza ndoto yake ya kuwa balozi wa mazingira kwa kutumia elimu anayoipata kutoka TFS Septemba 10,2025.
TFS ni taasisi ya serikali iliyopewa jukumu la kusimamia na kuhifadhi rasilimali za misitu nchini huku majukumu yake makuu yakiwa ni,Kuhifadhi na kulinda misitu ya hifadhi pamoja na maeneo nyeti ya ikolojia,Kuotesha na kugawa miche kwa wananchi ili kuongeza kiwango cha upandaji miti na kupunguza ukataji holela, Kuwezesha fursa za kiuchumi kupitia misitu, kama vile biashara ya miche, mbao, matunda na mazao mengine ya misitu na Kuchangia mapambano dhidi ya mabadiliko ya tabianchi kwa kuhakikisha miti inapandwa kwa wingi na misitu inalindwa.
Kupitia ushirikishwaji huu, TFS si tu inalinda misitu, bali pia inatoa mwanga mpya wa kiuchumi kwa wananchi wa Kishapu na maeneo mengine nchini.
Mkazi wa Mtaa wa Maendeleo Wilayani Kishapu Mkoani Shinyanga Lucas Alex akizungumzia namna elimu ya TFS imewafungulia fursa mpya za kiuchumi kupitia uandaaji na uuzaji wa miche Septemba 10,2025.
Mkazi wa Mtaa wa Mwamashele Kata ya Kishapu Wilayani Mkoani Shinyanga Zacharia Heche akitengeneza viliba vya kupandia miche Septemba 10,2025

Ameongeza kuwa wamepata elimu ya jinsi ya kuandaa mashimo yatakayopelekea mmea kustawi na kukuwa na jinsi ya kuandaa mchanga,udongo na samadi kwenye mche tofauti na elimu za mitaani ambazo hazina utalamu kiasi Cha kupelekea miche kufa.
Kwa upande wake, Gidion Mathias, mwanafunzi wa kidato cha pili Wilayani humo amesema anatamani kuwa balozi wa mazingira kwa kujifunza zaidi namna ya kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi kupitia elimu anayoipata kutoka TFS kwa masaa ya ziada akiwaendea.
Akizungumzia mikakati ya taasisi hiyo, Mhifadhi Misitu wa Wilaya ya Kishapu, Tumaini Masatu Mwijarubi, amesema katika mwaka wa fedha 2025/2026 TFS Kishapu imelenga kuotesha miche 200,000 ya matunda, mbao na kivuli, ambayo itagawiwa bure kwa wananchi wakati wa msimu wa mvua utakapoanza.
“Serikali imeamua kusaidia wananchi kwa kuondoa vikwazo vya gharama za ununuzi wa miche. TFS tumekabidhiwa jukumu la kuotesha na kugawa miche hiyo bure, huku gharama zikibebwa na serikali. Lengo letu ni kuhakikisha kila mwananchi anashiriki katika kuhifadhi mazingira,” amesema Mwijarubi.
Aidha, amebainisha kuwa TFS itaendelea kushirikisha wananchi si tu kwa ajili ya upandaji miti, bali pia kuwajengea uwezo wa utunzaji misitu, ili kuongeza ushiriki wao katika mnyororo wa thamani wa zao la misitu.
Mwanafunzi wa kidato cha pili Gidion Mathias akieleza ndoto yake ya kuwa balozi wa mazingira kwa kutumia elimu anayoipata kutoka TFS Septemba 10,2025.TFS ni taasisi ya serikali iliyopewa jukumu la kusimamia na kuhifadhi rasilimali za misitu nchini huku majukumu yake makuu yakiwa ni,Kuhifadhi na kulinda misitu ya hifadhi pamoja na maeneo nyeti ya ikolojia,Kuotesha na kugawa miche kwa wananchi ili kuongeza kiwango cha upandaji miti na kupunguza ukataji holela, Kuwezesha fursa za kiuchumi kupitia misitu, kama vile biashara ya miche, mbao, matunda na mazao mengine ya misitu na Kuchangia mapambano dhidi ya mabadiliko ya tabianchi kwa kuhakikisha miti inapandwa kwa wingi na misitu inalindwa.