` MSAADA WA MATIBABU YA MGUU

MSAADA WA MATIBABU YA MGUU

MSAADA WA MATIBABU YA MGUU

Na Mwandishi Wetu

Ibrahimu Masunga Mayuma mkazi wa Ngokolo Manispaa ya Shinyanga.

Anaomba msaada wa matibabu ya mguu wake,pamoja na magongo ya kutembelea ili asiendelee kupata maumivu.

Anaeleza kuwa, Mguu wake kwa mujibu wa Madaktari kwamba una Kansa na unatakiwa kukatwa,lakini kwa sasa amewekewa chuma ndani ya mguu wake, chuma ambayo anadai ina muumiza na imetengeza shimo na kutoa maji muda wote, shimo hilo kwa sasa ameliziba na daso.

Anasema anapokuwa akitembea anasikia maumivu makali, ambapo anaomba msaada wa kupata magongo ya kutembelea.

Kwa msaada zaidi wasiliana na mdogo wake Masunga 
Mayuma


Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464