Na Marco Maduhu,SHINYANGA
SHULE ya Awali na Msingi Mwenge iliyopo manispaa ya Shinyanga, imekuwa ikifanya vizuri kitaaluma,ambapo ndani ya miaka 10 mfululizo imefaulisha wanafunzi kwa asilimia 98.
Hayo yamebainishwa leo na Mwalimu Mkuu wa shule hiyo Hassan Hemed,wakati akisoma taarifa ya shule kwa mgeni rasmi kwenye mahafali ya wahitimu wa darasa la Saba shuleni hapo.
Amesema shule hiyo nikongwe na imekuwa ikifanya vizuri kitaaluma,na kwamba ndani ya miaka 10 mfululizo kuanzia 2015 hadi 2024 imefaulisha wanafunzi kwa asilimia 98.

"Ndugu Mgeni Rasmi shule ya Awali na Msingi Mwenge tumefanikiwa kufikia ufaulu wa wanafunzi kwenye mitihani ya kitaifa kwa zaidi ya asilimia 98 ndani ya miaka 10 mfululizo." amesema Hemed.
Ameongeza pia kupitia utoaji wa chakula shuleni wamefanikiwa kuwa na mahudhurio ya wanafunzi kwa asilimia 99.
Aidha,amebainisha baadhi ya changamoto ambazo zinaikabili shule hiyo kuwa ni uhaba wa matundu ya vyoo,madawati,ukarabati wa celling board za vyumba vitano vya madarasa, ukosefu wa umeme kwenye majengo ya nane na photocopy mashine.
Kwa upande wake Mgeni Rasmi kwenye mahafali hayo mdau wa elimu Salum Kitumbo, amewapongeza Walimu wa Shule hiyo kwa ufundishaji mzuri na kufaulisha wanafunzi.
Amesema yeye kama mdau mkubwa wa elimu ataendelea kuwa nao bega kwa bega,pamoja na kutafuta ufumbuzi wa changamoto moja baada ya nyingine ambazo zinaikabili shule hiyo.
Amempongeza pia Rais Dk.Samia Suluhu Hassan,kwa kuendelea kutoa fedha na kuboresha miundombinu ya elimu ambapo watoto wamekuwa wakisoma katika mazingira rafiki na kufanya vizuri kitaaluma.
TAZAMA PICHA👇👇
Mdau wa Elimu Salum Kitumbo akizungumza kwenye mahafali ya shule ya Awali na Msingi Mwenge Manispaa ya Shinyanga.
Mwalimu Mkuu wa Shule ya Awali na Msingi Mwenge Manispaa ya Shinyanga Hassan Hemed akizungumza.
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464