` TUME YA HAKI ZA BINADAMU YAWANOA POLISI NA WAANDISHI WA HABARI MKOA WA MWANZA

TUME YA HAKI ZA BINADAMU YAWANOA POLISI NA WAANDISHI WA HABARI MKOA WA MWANZA


Edwin Soko

Mwanza

Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora imetoa mafunzo Kwa Jeshi la Polisi na Waandishi wa Habari Mkoa wa Mwanza ili waweze kuheshimu haki za binadamu kuelekea uchaguzi Mkuu Oktoba 29, 2025.


Akifungua mafunzo hayo Afisa Tawala Mkoa wa Mwanza Bwana Balandya Elikana alisema kuwa, Jeshi la Polisi na Waandishi wa Habari Wana wajibu wa kutimiza wajibu wao Kwa kuzingatia haki za binadamu na utawala Bora.

Alikana aliongeza kuwa ili uchaguzi uwe huru na wa haki ni lazima haki za binadamu zizingatiwe na wananchi watumie vyema haki zao kwenye uchaguzi mkuu ujao.

" Waandishi wa habari wana jukumu kubwa la kuhabarisha umma juu ya umuhimu wa kuheshimu haki za binadamu na misingi ya utawala Bora kuelekea uchaguzi mkuu" alisema alikana.

Salamau za Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora zilizosomwa na Bibi Saumu Mgeni, Afisa wa Tume ofisi ya Mwanza, zilisisitiza kuwa, mafunzo hayo ya siku moja yanalenga kuongeza uelewa Kwa Polisi juu ya haki za binadamu kuelekea uchaguzi mkuu pamoja na kuhakikisha Jeshi linazingatia haki za binadamu na utawala Bora.

Naye Bwana Yohana Tumaini Mchalo, Afisa toka Tume ya Haki za Binadamu na utawala Bora alisema kuwa, Jeshi la Polisi lina dhamana kubwa kuelekea uchaguzi mkuu wa Oktoba 29, 2025.

Mchalo aliwapitisha washiriki kwenye mikataba ya kimataifa, katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na sheria mbalimbali na kuwataka washiriki kutambua mikataba hiyo na kuzingatia haki za binadamu kwenye utendaji wao wa Kila siku.

Mafunzo hayo yalijumuisha Maafisa wa Polisi na Askari wapatao arobaini toka ofisi ya OCD za Ilemela na Nyamagana Jijini Mwanza pamoja na waandishi wa habari ishirini toka Mkoa wa Mwanza.

Pia Kwa mujibu wa Bwana Yohana Mchalo alibainisha kuwa, mafunzo hayo yanafanyika kwenye Mikoa kumi na nne ya Tanzania Bara na Mikoa mitano ya Tanzania Visiwani.
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464