Mkufunzi wa mafunzo hayo, Kadama Malunde, ambaye pia ni mwandishi wa habari, amesisitiza kuwa ulinzi huanzia kwa mwandishi mwenyewe. Ameeleza umuhimu wa kulinda vifaa vya kazi, kutumia nywila imara, kuepuka viunganishi visivyo salama, na kuweka uthibitishaji wa hatua mbili (Two-Factor Authentication), hasa kuelekea Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2025.
Mafunzo haya ni sehemu ya mradi wa “Empowering Journalists for Informed Community” unaofadhiliwa na Umoja wa Ulaya (EU) na Shirika la Maendeleo la Uswisi (SDC), na kutekelezwa na International Media Support (IMS), Union of Tanzania Press Clubs (UTPC) na JamiiAfrica.
Soma pia : WAANDISHI WA HABARI SHINYANGA WAELIMISHWA MBINU ZA KUJILINDA