` VIONGOZI WA UWT-SHINYANGA MJINI WAFUNDWA

VIONGOZI WA UWT-SHINYANGA MJINI WAFUNDWA



Mwenyekiti wa UWT wilaya ya Shinyanga Rehema Nhamanilo akizungumza kwenye mafunzo ya makatibu wa UWT kutoka kata na matawi

Suzy Butondo, Shinyanga 

Mwenyekiti wa UWT wilaya ya Shinyanga amewataka viongozi wanawake wote kuondoa makundi yaliyokuwa kwenye uchaguzi wa kura za maoni, badala yake wapendane washirikiane ili kuhakikisha ushindi wa kishindo unapatikana ndani ya CCM.

Hayo ameyasema leo kwenye kikao kazi cha kuimalisha umoja wa wanawake  kwa Wenyeviti  makatibu kata, matawi, madiwani wateule viti  maalumu na madiwani wa kata wanawake, ambapo amesema kila mmoja  awe na upendo na mwenzake na kuhakikisha wanashirikiana kwa pamoja katika kuleta ushindi.

Muda huu tulionao kwa sasa sio wa kukaa na kuendelea kulaumiana, tunatakiwa kuungana kwa pamoja kuweza kuzitafuta kura za Rais, mbunge na diwani, muda wa makundi umeisha sasa hili ni la kwetu sote hatuna budi kuungana na kuwa wamoja,amesema Nhamanilo.

Katibu wa chama cha mapinduzi CCM wilaya ya Shinyanga Hamisa Chacha amewataka wanawake wote wa UWT waache kudhuliana maneno ambayo hayaleti amani badala yake wasameheane na kuhakikisha wanaungana kwa pamoja katika kuleta ushindi ndani ya CCM.

,Niwaombe sana viongozi wenzangu tushirikiane kwa pamoja, kwani tumeshawapata madiwani wa kupeperusha bendera ya CCM na tumempata mbunge na Rais hivyo hao ndio tushirikiane nao ili kuhakikisha tunapata ushindi kwa kishindo na kila kiongozi asimame kwenye nafasi yake na asiwepo wa kuonewa,amesema Chacha.

Kwa upande wake katibu wa UWT wilaya ya Shinyanga mnjini Getrude Mboyi amewashauri wanawake wote kuwa na mkakati mmoja, na alisisitiza upendo na mshikamano uendelee,ikiwa ni pamoja na kufuata maelekezo yote waliyopewa ya kiuongozi .
Aidha Mboyi amewasisitiza viongozi wote wa UWT wilaya ya Shinyanga mjini, kwamba katika wakati huu wa kuelekea uchaguzi mkuu wa mwaka 2025 wahakikisha wanatimiza majukumu yao yote yanayotakiwa kutimizwa, ili kuhakikisha CCM inapata ushindi.

,Niwaombe tu viongozi wenzangu, wenyeviti, makatibu na madiwani wateule  mkitoka hapa mkatimize majukumu yenu, kila mmoja aitendee haki nafasi yake,kwani kila mmoja hapa anajua majukumu yake, hivyo niwaombe kila mmoja asimamie nafasi  yake kikamilifu,amesema Mboyi.
Mwenyekiti wa UWT wilaya ya Shinyanga Rehema Nhamanilo akizungumza kwenye mafunzo ya makatibu wa UWT kutoka kata na matawi
Mwenyekiti wa UWT wilaya ya Shinyanga Rehema Nhamanilo akitoa mafunzo kwenye mafunzo ya makatibu wa UWT kutoka kata na matawi
Katibu wa Chama Cha Mapinduzi CCM Shinyanga mjini Hamisa Chacha akizungumza kwenye mafunzo ya viongozi wa UWT wilaya
Katibu wa Chama Cha Mapinduzi CCM Shinyanga mjini Hamisa Chacha akizungumza kwenye mafunzo ya viongozi wa UWT wilaya




Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464