` UTT AMIS YAZINDUA TAWI JIPYA KAHAMA

UTT AMIS YAZINDUA TAWI JIPYA KAHAMA

Mkuu wa Wilaya ya Kahama, Mhe. Frank Nkinda na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa UTT AMIS, Prof. Faustine Kamuzora (kulia) wakikata utepe ishara ya uzinduzi wa Tawi ya UTT AMIS - Kahama Mkoani Shinyanga

Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

Kampuni ya Uwekezaji ya UTT Asset Management and Investor Services (UTT AMIS) imezindua tawi jipya mjini Kahama mkoani Shinyanga, hatua inayolenga kusogeza karibu huduma za kifedha na uwekezaji kwa wananchi.

Hafla fupi ya Uzinduzi wa kituo hicho cha Investor Services imefanyika leo Jumatano Agosti 20,2025 ikiongozwa na Mkuu wa Wilaya ya Kahama, Mhe. Frank Nkinda, ambaye amesema ufunguzi wa tawi hilo ni kielelezo cha dhamira ya UTT AMIS kupanua huduma zake na kuwawezesha wananchi kupata elimu ya fedha, akiba na uwekezaji kwa urahisi zaidi.

“Ni matumaini yangu UTT AMIS itaendelea kuja na huduma bunifu na kusogeza zaidi huduma hizi kwa wananchi wa Kahama na maeneo ya jirani. Serikali inatambua kuwa maendeleo ya uchumi na kupunguza umaskini haviwezi kufanikishwa bila ushiriki wa wananchi mmoja mmoja,” amesema Mhe. Nkinda.

Amefafanua kuwa kuanzishwa kwa UTT AMIS ni sehemu ya mkakati wa Serikali wa kuwawezesha Watanzania kushiriki katika umiliki wa uchumi kupitia uwekezaji katika masoko ya fedha na mitaji, akisisitiza kuwa uwekezaji wa muda wa kati na mrefu utawasaidia wananchi kupata mitaji kwa shughuli nyingine za kiuchumi kama kilimo, ufugaji na biashara.

Mhe. Nkinda amewataka wananchi wa Kahama na Shinyanga kwa ujumla kutumia ipasavyo fursa zinazotolewa na UTT AMIS.

“Sasa ni wakati wa wakulima, wafugaji, wachimbaji wa madini, vijana na wafanyabiashara kuchangamkia huduma hizi ili kuongeza kipato na kukuza uchumi wa familia na taifa”,amesema. 

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa UTT AMIS, Prof. Faustine Kamuzora, amesema tangu kuanzishwa kwake, taasisi hiyo inasimamia rasilimali zenye thamani ya zaidi ya shilingi trilioni 3.5, ikihudumia karibu wawekezaji 500,000 kupitia mifuko mbalimbali inayotoa faida ya wastani wa asilimia 12–15 kwa mwaka kulingana na mwenendo wa soko.

“Kila mmoja anaweza kuwekeza , iwe ni mtu binafsi, kikundi, kampuni au taasisi. Unaweza kuanza kwa kiasi kidogo kuanzia shilingi 5,000 au 10,000, na kufanya miamala kwa njia za simu au benki. Hata ukihitaji kutoa fedha zako, unaweza kufanya hivyo ndani ya siku tatu hadi kumi kutegemea mfuko uliowekeza,” amesema Prof. Kamuzora.

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa UTT AMIS, Simon Migangala, ameishukuru Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuweka mazingira rafiki ya uwekezaji.

 Amesisitiza kuwa maendeleo ya teknolojia yamechangia kurahisisha huduma, kwani sasa mteja anaweza kuwekeza au kutoa fedha kupitia simu ya mkononi akiwa popote na muda wowote.

Kwa sasa UTT AMIS tayari ina matawi katika mikoa ya Mwanza, Mbeya, Arusha, Dodoma na Zanzibar, na tawi la Kahama limefunguliwa katika eneo la kibiashara lenye fursa kubwa za kiuchumi.
Mkuu wa Wilaya ya Kahama, Mhe. Frank Nkinda na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa UTT AMIS, Prof. Faustine Kamuzora (kulia) wakikata utepe ishara ya uzinduzi wa Tawi ya UTT AMIS - Kahama  Mkoani Shinyanga Agosti 20,2025 - Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog 
Mkuu wa Wilaya ya Kahama, Mhe. Frank Nkinda na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa UTT AMIS, Prof. Faustine Kamuzora (kulia) wakikata utepe ishara ya uzinduzi wa Tawi ya UTT AMIS - Kahama  Mkoani Shinyanga Agosti 20,2025

Mkuu wa Wilaya ya Kahama, Mhe. Frank Nkinda akionesha nyaraka baada ya kufungua akaunti wakati wa uzinduzi wa Tawi ya UTT AMIS - Kahama  Mkoani Shinyanga
Mkuu wa Wilaya ya Kahama, Mhe. Frank Nkinda akionesha nyaraka baada ya kufungua akaunti wakati wa uzinduzi wa Tawi ya UTT AMIS - Kahama  Mkoani Shinyanga
Mkuu wa Wilaya ya Kahama, Mhe. Frank Nkinda akizungumza wakati wa uzinduzi wa Tawi ya UTT AMIS - Kahama  Mkoani Shinyanga

 Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa UTT AMIS, Prof. Faustine Kamuzora akizungumza wakati wa uzinduzi wa Tawi ya UTT AMIS - Kahama  Mkoani Shinyanga

Mkurugenzi Mtendaji wa UTT AMIS, Simon Migangala, akizungumza wakati wa uzinduzi wa Tawi ya UTT AMIS - Kahama Mkoani Shinyanga

Mkuu wa Wilaya ya Kahama, Mhe. Frank Nkinda na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa UTT AMIS, Prof. Faustine Kamuzora (kushoto) wakizungumza jambo ndani ya Kituo cha UTT AMIS - Kahama  Mkoani Shinyanga

Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464