` MTAKUWWA AWAMU YA II KUZIBA MWANYA WA UKATILI KISHAPU

MTAKUWWA AWAMU YA II KUZIBA MWANYA WA UKATILI KISHAPU

 Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu ambaye pia ni Mwenyekiti wa MTAKUWWA Wilayani humo akizungumza kwenye uzinduzi wa Mpango wa Taifa wa Kutokomeza Ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto Agosti 14,2025 Katika Ukumbi wa Halmshauri hiyo

Na Sumai Salum-Kishapu

Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu Mkoani Shinyanga imezindua Mpango wa Pili wa Taifa wa Kutokomeza Ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto (MTAKUWWA II),

Akizungumza katika uzinduzi huo,Mkurugenzi Mtendaji wa Hamashauri ya Wilaya ya Kishapu ambaye pia ni Mwenyekiti wa MTAKUWWA ngazi ya Wilaya Emmanuel Johnson, Agosti 14,2025 kwenye Ukumbi wa Halmashauri hiyo amewasisitiza wajumbe wote umuhimu wa kutekeleza majukumu yao kwa uzito mkubwa.

Ameshauri kwamba utekelezaji madhubuti wa wajibu huo ni msingi wa kuhakikisha ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto unatokomezwa.

Ameongeza kuwa Halmashauri itaandaa na kutenga bajeti maalum kwa ajili ya kuwasaidia wahanga wa ukatili pindi inapohitajika. Kauli hii inaashiria dhamira ya Halmashauri katika kutoa msaada wa kifedha na kiutatuzi kwa walioathiriwa, kuhakikisha wanapokea msaada unaohitaji kwa wakati unaofaa, hasa katika hali za dharura.

Afisa Maendeleo Mkoani Shinyanga ambaye pia ni Katibu wa MTAKUWWA ngazi ya Mkoa Bestina Gunje akiwasilisha mpango wa mkoa kwenye uzinduzi wa Mpango wa Taifa wa Kutokomeza Ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto Wilayani Kishapu Agosti 14,2025 Katika Ukumbi wa Halmshauri hiyoAfisa Maendeleo Wilayani Kishapu Mkoani Shinyanga ambaye pia ni Katibu wa MTAKUWWA Wilayani humo Joseph Swalala akizungumza kwenye uzinduzi wa Mpango wa Taifa wa Kutokomeza Ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto Agosti 14,2025 Katika Ukumbi wa Halmshauri hiyo

Johnson ameendelea kuonya vikali tabia ya kuwatumikisha Watoto katika shughuli za kuingizia kipato familia au kuwatumia kama nguvu kazi kwenye mashamba ya familia wakati wa masomo amesisitiza kuwa vitendo hivyo havikubaliki na ni kinyume cha sheria ya nchi na haki za Mtoto, hivyo hatua za kisheria zitafuata dhidi ya wote wanaoshiriki au kuruhusu mbinu kama hizo.

“Wajumbe wa MTAKUWWA kila mmoja anatakiwa kutimiza wajibu wake kikamilifu ili kuisaidia jamii kuondokana na ukatili" Amesema Johnson

Aidha, wawezeshaji wa Mpango Kazi wa MTAKUWWA II ngazi ya Wilaya na Mkoa wamewasilisha mienendo na maelezo ya utekelezaji wa mpango huo katika awamu ya kwanza na kuelezea mikakati ya awamu ya pili.

MTAKUWWA II ngazi ya Wilaya inamipango nane ikiwa ni pamoja na Kuimalisha Uchumi wa Kaya,Kuonda mila na desturi kandamizi,Mazingira salama maeneo ya Umma,Mazingira salama katika Teknolojia ya habari na mawasiliano,Malezi chanya,Utekelezaji na usimamizi wa sheria,Huduma za mwitikio kwa wahanga na manusura wa ukatili Mazingira salama Shuleni na stadi za maisha pamoja na Uratibu,Ufuatiliaji na Tathmini.

Mpango huu ulivyozungumzwa ngazi za Taifa

Naibu Waziri Mwanaidi amesema kwamba MTAKUWWA II unalenga kupunguza ukatili dhidi ya wanawake na watoto kwa asilimia 50, akitoa mwongozo wa kuanzisha kamati ngazi ya Wilaya, Kata na Mtaa kama sehemu ya mpango huo.

Pia, Wizara ya Katiba na Sheria imethibitisha kushirikiana na wadau mbalimbali kuhakikisha haki kwa wanawake na watoto inapatikana kwa ufanisi kupitia mpango huu.

Taarifa ya Utekelezaji MTAKUWWA 2024/2025 ngazi ya Wilaya inaonesha kuwepo kwa lamli chonganishi zinazopelekea kutokea kwa ukatili pia wamebaini baadhi ya mazingira kuwa hatarishi ikiwa ni pamoja na Watoto kuchunga mifugo wakati wa masomo na uwepo wa ngoma za asili zinazopelekea ukatili mbalimbali kufanyika hasa Kata za Ukenyenge,Talaga na Songwa huku kesi 35 za ukatili zikitolewa taarifa kwenye vyombo vya kisheria ikiwemo migogoro ya familia, mimba kwa mwanafunzi mmoja na vipigo kwa Wanawake na Watoto wadogo

Mwakilishi wa kundi la Wanawake Fredina Said ameshauri kamati ya mtakuwa iendelee kutoa elimu ya kujitambua na kuwajengea uelewa wa pamoja wanawake kundi ambalo limekuwa waathirika wa moja kwa moja wa matukio ya ukatili wakiwa ndio walezi wakuu wa familia.

Kikao hicho kilichojumuisha wajumbe wa mtandao huo kutoka ngazi ya Wilaya kimemalizika kwa shukrani za pamoja kwa serikali na watendaji ngazi zote kwa uwajibikaji mkubwa uliopelekea kuonesha matokeo chanya hadi sasa kwenye jamii ya Kishapu.
Mratibu mradi wa Chaguo langu haki yangu na mwezeshaji MTAKUWWA Wilayani Kishapu Mkoani Shinyanga Juma Ndoera akiwaslisha mada ya mpango wa pili MTAKUWWA ngazi ya Wilaya kwenye uzinduzi wa Mpango wa Taifa wa Kutokomeza Ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto Agosti 14,2025 Katika Ukumbi wa Halmshauri hiyoAfisa Program Kutoka Wildaf Rachel Zerno akizungumza kwenye uzinduzi wa Mpango wa Taifa wa Kutokomeza Ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto Wilayani Kishapu Agosti 14,2025 Katika Ukumbi wa Halmshauri hiyoMwakilishi kutoka kundi la Wanawake Wilayani Kishapu Mkoani Shinyanga Fredina Said akizungumza kwenye uzinduzi wa Mpango wa Taifa wa Kutokomeza Ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto Agosti 14,2025 Katika Ukumbi wa Halmshauri hiyo
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464