
Msaada huo unajumuisha vitanda 20, magodoro 20, mashuka na foronya 100 pamoja na vifaa mbalimbali vya usafi.
Makabidhiano hayo yamefanyika Agosti 9,2025 katika viwanja vya hospitali hiyo, yakiongozwa na Kaimu Mkurugenzi wa Rasilimali Watu wa CRDB, Ndg. Matungwa Babyega, akiwa ameambatana na Meneja wa Kanda ya Magharibi, Ndg. Jumanne Wagana, pamoja na viongozi wengine kutoka makao makuu na ofisi za kanda.
Vifaa hivyo vimepokelewa na Mganga Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Dkt. Yudas Ndungile, kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga.
Akipokea msaada huo, Dkt. Ndungile ameishukuru Benki ya CRDB kwa mchango wao muhimu katika kuboresha huduma za afya, akisisitiza kuwa vifaa hivyo vitasaidia kupunguza changamoto ya upungufu wa vitanda na magodoro hospitalini hapo.