
Katibu wa CCM wilaya ya Kahama Andrew Chatwanga ametaja matokeo kwenye majimbo matatu kwa nafasi za ubunge kwa majimbo matatu ya msalala,kahama na ushetu.Ambapo Msalala wagombea walikuwa sita na wajumbe 7845 na kura halali zilizopigwa 7685 na zilizohalibika ni 160.
Ambapo Mabula Magangila aliongoza nakupata kura 5518,Ambrose Nangale kura 929,Simon Lufyega kura 189, Ezeckiel Maige kura 791,Edson Masondole kura 152 na Emanuel Shiganza Kura 105.
Chatwanga amesema waliopigiwa kura wajumbe kwa Kahama mjini walikuwa 6193 na kura 80 zilihalibika na halali kura ni 6113 ambapo aliyeongoza ni Benjamini Ngaiwa alipata kura 2093, Sweetbert Nkuba kura 1389, Jumanne Kishimba kura 1144,
Francis Mihayo kura 821 na James Lembeli kura 219, Juliana Kajala kura 256.
Chatwanga amesema jimbo la Ushetu Emanuel Cherehani aliongoza alipata kura 5656, Machibya Mwambilija kura 171 ,Valerian Mwambasha alipata kura 153 Musa Misungwi alipata kura 452 na zoezi la kupiga kura za maoni kata tatu kati ya 20 zilizopo ikiendelea.
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464