` RUWASA,KUWASA WAPEWA SHIME NA MWENGE WA UHURU USHIRIKIANO UTEKELEZAJI MIRADI YA MAJI

RUWASA,KUWASA WAPEWA SHIME NA MWENGE WA UHURU USHIRIKIANO UTEKELEZAJI MIRADI YA MAJI


RUWASA,KUWASA WAPEWA SHIME NA MWENGE WA UHURU USHIRIKIANO UTEKELEZAJI MIRADI YA MAJI

Na Marco Maduhu,KAHAMA

KIONGOZI wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa Ismail Ali Ussi,amewapongeza Wakala wa Maji safi na Usafi wa Mazingira (RUWASA)Mkoa wa Shinyanga kwa kushirikiana vyema na Mamlaka ya Maji Kahama (KUWASA)kutekeleza miradi ya Maji.
Amebainisha hayo leo Agosti 3,2025 wakati akiweka jiwe la Msingi kwenye ujenzi wa Mradi wa Chujio la Maji Mwendakulima wilayani Kahama.

Amesema,anawapongeza RUWASA pamoja na KUWASA namna wanavyofanya kazi kwa ushirikiano mzuri kutekeleza miradi ya maji safi kwa wananchi.
"Wizara ya Maji inafanya kazi nzuri sana, nampongeza pia Waziri wa Maji Jumaa Aweso anafanya kazi nzuri ya kumsaidia Rais Samia Suluhu Hassan kupeleka huduma ya maji kwa wananchi kupitia Mamlaka za Maji na Wakala wa Maji RUWASA,"amesema Ussi.

Aidha,amesema mradi huo ni Baba Lao na hua hana shaka na miradi ya maji sababu hua inatekelezwa kwa ufanisi na ubora wa hali ya juu na kuwaondolea adha wananchi ya ukosefu wa huduma ya maji.
"Tumepitia nyaraka mbalimbali za mradi huu hakuna ubabaishaji na Mwenge wa Uhuru umeridhia kuweka Jiwe la Msingi,"amesema Ussi.

Naye Mkuu wa wilaya ya Kahama Frank Nkinda,amesema mradi huo utakapokamilika wilaya hiyo itakuwa na Maji ya kutosha na kuendelea kutoa huduma bora kwa wananchi.
Awali Mkurugenzi wa Uzalishaji na Usambazaji wa Maji (KUWASA)Mhandisi Magige Marwa, akisoma taarifa ya mradi huo, amesema Manispaa ya Kahama inategemea chanzo kimoja cha maji ambacho ni Ziwa Victoria.

Anasema, katika kuhakikisha huduma ya Majisafi na Salama ina imarika na kupatikana wakati wote uongozi wa Mgodi wa Barrick Buzwagi ulitoa miundombinu na kuvuna na kuhifadhi maii ya mvua, kwa kushirikiana na KUWASA kufanya kazi ya usanifu wa miundombinu ya kusafisha na kusafirisha maji hayo kwenda Tenk la kuhifadhia maji Shunu.
"Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa ujenzi wa Mradi huu wa Chujio la Maji gharama zake ni Sh.bilioni 4.8 ambapo una jumuisha ununuzi wa viungio,vifaa vya ujenzi, na mabomba ya maji," amesema Mhandisi Marwa.

Amesema,mradi wa ujenzi wa Chujio hilo la Maji Mwendakulima unatazamiwa kuhudumia zaidi ya asilimia 66 ya wakazi waishio Manispaa ya Kahama.

Ameongeza kuwa choteo la kuvunia maji ya mvua lina ukubwa wa Hekta 75,Bwawa lenye uwezo wa kuhifadhi Maji Lita Milioni 1.5 na Mfumo wa kusafisha na kuchuja maji wenye uwezo wa kuchuja lita za maji Milioni 10 kwa siku.
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464