` AZZA HILLAL HAMAD ACHUKUA FOMU ZA UTEUZI KUGOMBEA UBUNGE JIMBO JIPYA LA ITWANGI KUPITIA CCM UCHAGUZI MKUU 2025

AZZA HILLAL HAMAD ACHUKUA FOMU ZA UTEUZI KUGOMBEA UBUNGE JIMBO JIPYA LA ITWANGI KUPITIA CCM UCHAGUZI MKUU 2025

Na Marco Maduhu,SHINYANGA

Azza Hillal Hamad,amechukua fomu za Uteuzi kugombea Ubunge Jimbo Jipya la Itwangi kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM)katika Uchaguzi Mkuu 2025.
Amechukua Fomu hizo leo Agost 24,2025 katika Ofisi za Mkurugenzi wa Halmashauri ya Shinyanga kwa msimamizi wa uchaguzi Jimbo la Itwangi na Solwa Joseph Ntomela,huku akisindikizwa na Wanachama pamoja na Wananchi wa Itwangi.

Azza akizungumza mara baada ya kuchukua Fomu hizo, ameishukuru Kamati Kuu ya Halmashauri ya CCM Taifa kwa kupitisha jina lake kugombea Ubunge katika Jimbo hilo la Itwangi, na kwamba nafasi hiyo ataiwakilisha vyema kwa CCM kupata Ushindi wa kishindo, pamoja na kura nyingi za Rais Dk.Samia Suluhu Hassan.
Amewashukuru pia wana CCM wa Itwangi kwa kumpatia nafasi hiyo baada ya kushinda kwenye kura za maoni ndani ya Chama, na kwamba hatowaangusha bali ataitendea haki nafasi hiyo.

Aidha,amewasihi wana CCM kuvunja makundi baada ya kupatikana Mgombea Mmoja,bali wote wawe kitu kimoja kwa kupeperusha bendera ya CCM katika Uchaguzi Mkuu wa 2025 kwa kupata ushindi kwa Madiwani,Wabunge na Rais Samia.
“Mimi kwa leo sina mengi ya kuzungumza. Nimekuja tu kuchukua fomu ya uteuzi, nitazungumza kwa kina wakati wa kampeni,” amesema Azza.

Nao baadhi ya wananchi wa Itwangi akiwamo Regina Peter, wamesema wanafuraha jina la Azza kurudi,sababu wanamjua katika uzoefu wake wa kuchapaka kazi kipindi alipokuwa Mbunge wa Vitimaalum, na wanaimani naye katika kuwaletea maendeleo.

TAZAMA PICHA👇👇
Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Itwangi na Solwa Joseph Ntomela (kulia)akimkabidhi Azza Hillal Hamad Fomu za Uteuzi kugombea Ubunge Jimbo la Itwangi.
Mheshimiwa Azza Hillal Hamad akionyesha Fomu za Uteuzi kugombea Ubunge Jimbo la Itwangi Uchaguzi Mkuu 2025.
Mheshimiwa Azza Hillal Hamad akisalimiana na wananchi wa Itwangi mara baada ya kuchukua Fomu za Uteuzi kugombea Ubunge katika Jimbo la Itwangi.





Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464