Na Marco Maduhu,SHINYANGA
SERIKALI imewataka ndugu wa Watu 20 ambao wamesalia kuokolewa baada ya kufukiwa na Mgodi katika Machimbo ya Nyandolwa wilayani Shinyanga, kwamba wasikate tamaa,na kutaka Mgodi huo ubomolewe ili wachukue ndugu zao kwenda kuwazika.
Hayo yamebainishwa leo Agost 16,2025 na Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Julius Mtatiro,wakati akizungumza na ndugu wa watu hao 20 kabla ya kuwakaribisha Manaibu Waziri wa Sekta Mbili,kuzungumza na wananchi katika machimbo hayo.

Amesema,baadhi ya ndugu wamekuwa wakimpigia simu kumwambia waubomoe Mgodi huo,sababu wamechoka kusubili ndugu zao kuokolewa,wakidai siku zimekuwa nyingi tayari wameshariki.
"Niwaomba ndugu, muwe wavumilivu wakati serikali ikiendelea na zoezi la uokoaji, hatuwezi kuubomoa Mgodi," amesema Mtatiro.
Ameongeza kuwa,wala hawawezi kutumia mitambo mikubwa ya kisasa kufanya maokozi,bali wataendelea kutumia njia ya kienyeji,sababu kutumia mitambo mikubwa wataudidimiza mgodi wote na kuwaua hata kama wengine bado wapo hai.
Aidha,ametaja watu ambao wameokolewa na kuruhusiwa kwenda kwa ndugu zao baada ya kupona, kuwa ni Anthony Clement na Mayugula Japhet,huku Flano Peter akiendelea kupatiwa matibabu katika Hospitali ya Bugando Jijijini Mwanza.
Amewataja waliopoteza maisha, kuwa ni Emmanuel Kija na Magumba Ng'ondi,huku akibainisha kuwa tayari timu ya Wataalamu imeshabaini watu wengine wawili walipo,na muda wowote watawaokoa.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Daniel Sillo, amesema njia hiyo ya kienyeji kufanya uokoaji ni nzuri,sababu inaweza kuwakuta watu wengine wakiwa ni hai.
Amesema, wao wataendelea kuwapo kwenye tukio hilo,hadi hapo zoezi la uokoaji litakapo malizika, huku akiwasisitiza wananchi wawe na uvumilivu na serikali ipo pamoja nao.
Naibu Waziri wa Madini Steven Kisurwa, amesisitiza kasi iongezwe ya kufanya uokoaji, huku akitoa maagizo kusijefanyika tena njia hiyo ya ukarabati maduara matatu kwa wakati mmoja sababu ni hatari.