` PSSSF IMETOA TRILIONI 11.96 KULIPA MAFAO WANACHAMA WAKE

PSSSF IMETOA TRILIONI 11.96 KULIPA MAFAO WANACHAMA WAKE

PSSSF IMETOA TRILIONI 11.96 KULIPA MAFAO WANACHAMA WAKE

Na Marco Maduhu,DAR ES SALAAM

MFUKO wa Hifadhii ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF),umeshalipa jumla ya sh.Trilioni 11.96 kwa wanachama wake,tangu kuanzishwa kwake mwaka 2018.
Hayo yamebainishwa leo Agosti 14,2025 na Meneja wa Mafao kutoka PSSSF Ramadhani Mkenyenge,kwenye mkutano kati ya PSSSF na Wanachama wa Misa Tanzania, wakati akiwasilisha wasilisho la miaka saba ya PSSSF,Mafao na huduma zake.

Amesema mfuko huo ulianzishwa Agosti 1,2018 ukiwa na wanachama 862,986 na hadi kufika Juni 30 mwaka huu, wanajumla ya wanachama hai 807,010, na kwamba ndani ya miaka yake 7 tangu kuanzishwa kwake, wameshawalipa mafao wanachama wake jumla ya sh.Trilioni 11.96 kwa wanachama 348,909.
“Ndani ya miaka yetu 7 ya PSSSF,Mafao na huduma zake tumekuwa na mafanikio mengi sana na katika mwaka wa fedha 2025/2026 tunategemea kukusanya kiasi cha sh.bilioni 168.25 kwa mwezi sawa na ongezeko la asilimia 43.42 kutoka sh.bilioni 117.31,”amesema Mkenyenge.

Aidha,amesema pia wameendelea kuwalipa fedha zao mafao wastaafu kwa wakati, pamoja na kuhuisha taarifa zao kwa mfumo wa mtandao na hakuna tena kwenda PSSSF kupanga foleni.
Awali akizungumza kabla ya wasilisho hilo,amesema wapo tayari kufanya kazi na Misa Tanzania,ili kuhabarisha umma juu ya huduma za mfuko huo,huku akiwasisitiza waandishi wa habari wafanye kazi zao kwa weledi na kufanya uwiano wa habari.

Naye Mwenyekiti wa Misa Tanzania Edwin Soko,amewahakikishia PSSSF kwamba wataendelea kufanya nao kazi kwa ukaribu ili kuhabarisha umma juu ya huduma zote za PSSSF.
“ukiwa karibu na waandishi wa habari ume “solve” kila kitu, sababu waandishi ni daraja la kupeleka taarifa kwa jamii, sisi kama Misa Tanzania tunashukuru sana PSSSF kwa mashirikiano haya,”amesema Soko.

TAZAMA PICHA👇👇
Meneja wa Mafao kutoka PSSSF Ramadhani Mkenyenge akizungumza.
Meneja wa Mafao kutoka PSSSF Ramadhani Mkenyenge akizungumza.
Meneja wa Mafao kutoka PSSSF Ramadhani Mkenyenge akizungumza.
Afisa Uhusiano PSSSF Abdul Njaidi akizungumza.
Mwenyekiti wa Misa Tanzania Edwin Soko akizungumza.
Mwenyekiti wa Misa Tanzania Edwin Soko akizungumza.
Mkutano ukiendelea.

Picha za pamoja zikipigwa.
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464