` MWENGE WA UHURU WAZINDUA MRADI WA MAJI NTOBO "A"

MWENGE WA UHURU WAZINDUA MRADI WA MAJI NTOBO "A"


MWENGE WA UHURU WAZINDUA MRADI WA MAJI NTOBO "A"

Na Marco Maduhu,KAHAMA

WANANCHI zaidi ya 1,600 wa Kijiji cha Ntobo "A", Halmashauri ya Msalala wilayani Kahama, wameondokana na adha ya kutembea umbali mrefu kufuata maji, baada ya Mwenge wa Uhuru kuzindua rasmi mradi wa maji kijijini hapo.
Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa 2025, Ismail Ali Ussi, alizindua mradi huo leo Agosti 5, 2025, ikiwa ni sehemu ya miradi saba iliyozinduliwa, kuwekwa mawe ya msingi na kukaguliwa katika halmashauri hiyo, yenye jumla ya thamani ya sh.bilioni 1.

Akizungumza wakati wa uzinduzi huo,Ussi amesema Mwenge wa Uhuru umejiridhisha kuwa mradi huo umetekelezwa kwa viwango vya juu bila ubabaishaji, na umekuwa mkombozi mkubwa kwa wananchi.
“Mradi huu wa maji umewagusa wananchi wa Ntobo 'A', hasa kina mama waliokuwa wakiteseka kutafuta maji umbali mrefu. Sasa maji safi na salama yanapatikana karibu na makazi yao,” amesema Ussi.

Aidha, amewapongeza Wakala wa Majisafi na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA)Mkoa mzima wa Shinyanga kwa kusimamia vyema fedha za Serikali, chini ya uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan, na kuendelea kupeleka huduma za maji vijijini.
Meneja wa RUWASA wilaya ya Kahama,Mhandisi Maduhu Magili, awali akisoma taarifa ya mradi huo, amesema ulianza kutekelezwa Februari 18 mwaka huu na kukamilika Julai 7, kwa gharama ya Sh. milioni 88.3 kupitia Programu ya Malipo kwa Matokeo (PforR).

Amesema mradi huo umeondoa tatizo la muda mrefu la ukosefu wa huduma ya maji kwa wananchi wa Ntobo "A" na Hospitali ya Halmashauri ya Msalala, ambapo unahudumia jumla ya wananchi wapatao 1,612.

Nao baadhi ya wananchi wa Ntobo "A" wamesema mradi huo umekuwa mkombozi kwao hasa wanawake ambao ndiyo walikuwa wakipata shida ya kufuata maji umbali mrefu.

TAZAMA PICHA👇👇
Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa Ismail Ali Ussi akizungumza.
Meneja wa RUWASA wilaya ya Kahama Mhandisi Maduhu Magili akisima taarifa ya mradi.
Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa 2025 Ismail Ali Ussi akizindua mradi wa maji .
Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa 2025 Ismail Ali Ussi akizindua mradi wa maji .
Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa Ismail Ali Ussi akimpongeza Meneja wa RUWASA Mkoa wa Shinyanga Mhandisi Juliteh Payovela namna anavyosimamia utekelezwaji vizuri ya miradi ya Maji.
Picha za pamoja. zikipigwa.

Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464