` RC MBONI APOKEA MWENGE WA UHURU MKOA WA SHINYANGA

RC MBONI APOKEA MWENGE WA UHURU MKOA WA SHINYANGA

RC MBONI APOKEA MWENGE WA UHURU MKOA WA SHINYANGA

Na Marco Maduhu,SHINYANGA

MKUU wa Mkoa wa Shinyanga Mboni Mhita, amepokea Mbio za Mwenge wa Uhuru kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Tabora Paul Chacha.

Amepokea Mwenge huo leo Agosti 3,2025 katika Viwanja wa Stend ya Mabasi Kagongwa wilayani Kahama.

Amesema Mwenge huo wa Uhuru ukiwa Mkoani Shinyanga utakimbizwa umbari wa kilomita 819.2 ndani ya Halmashauri Sita na kupita katika miradi 44 kukagua,kuzindua na kuweka Mawe ya Msingi miradi yenye thamani ya sh.bilioni 17.3

Mbio hizo za Mwenge wa Uhuru,unakimbizwa na wakimbiza Mwenge Sita ,wakiongozwa na kiongozi Ismail Ali Ussi.

Kauli Mbiu ya Mwenge wa Uhuru mwaka huu inasema"Jitokeze kushiriki uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2025 kwa Amani na Utulivu.

Mwenge huo utakabidhiwa Mkoani Simiyu Agost 9,2025.

Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464