*****
Jamii ya wasukuma kutoka sanjo ya Busiya wametakiwa kujivunia mila desturi na tamaduni zao ambazo wamerithi kutoka kwa mababu kama sehemu ya kuzienzi na kuacha alama kwa vizazi vijavyo.
Hayo yamebainishwa na mtemi wa 24 wa busiya Ntemi Makwaiya wa tatu mwakati akizindua tamasha la utamaduni la sanjo ya busiya kwa mwaka 2025
Kwa upande wao Washiriki wa tamasha hilo kutoka vikundi mbalimbali vya ngoma za asili ya Kisukuma wameeleza tija ya uwepo wa matamasha hayo hususani kitunza mila la tamaduni zilizoachwa na mababu na kujikwamua kiuchumia kupitia michezo wanayoshiriki
Waratibu wa tamasha hilo na shuguli za utemi wa Busiya wamesema matamasha hayo yamekuwa yakisaidia kuwaunganisha jamii ya wasukuma kupitia michezo mbalimbali ambayo imekuwa ikijumuishwa katika tamasha hilo linalofanyika kwa mwaka wa 16 mfululizo
Tamasha la utamaduni limekuwa likitumika kama jukwaa la kuonyesha utamaduni wa msukuma kwa shuguli zinazofanywa ikiwemo Ngoma, mavazi ya asili ,michezo ya asili vyakula vya asili huku shughuli hizo zikitarajiwa kuhitinishwa July 7 mwaka huu katika viwanja vya utemi wa sanjo ya busiya wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464