Tanzia : ALIYEKUWA DIWANI WA KATA YA SOLWA AWADH HAFIZ AFARIKI DUNIA
Aliyekuwa Diwani wa Kata ya Solwa, Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga, Awadh Hafiz amefariki dunia baada ya kupata ajali ya bajaji aliyokuwa akisafiria kugongwa na basi la kampuni ya Frester.
Tukio hilo la kusikitisha limetokea Julai 19,2025 wakati marehemu akiwa safarini kutoka eneo la Kolandoto kuelekea Shinyanga Mjini, ambapo bajaji aliyopanda iligongana na basi hilo, na kusababisha majeraha makubwa yaliyosabisha kifo chake.
Chanzo MALUNDE BLOG