KATAMBI AENDELEA KUGUSA MAISHA YA WANANCHI WA SHINYANGA,AMKABIDHI MKANDARASI “SITE” UJENZI BARABARA YA LAMI MWAWAZA,STENDI YA MABASI KIZUMBI
Na Marco Maduhu,SHINYANGA
MBUNGE wa Jimbo la Shinyanga Mjini Patrobas Katambi,ambaye ni Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu,Kazi,Vijana,Ajira na watu wenye Ulemavu,amemkabidhi Mkandarasi eneo la ujenzi wa barabara ya Hospitali ya Mwawaza, na Ujenzi wa Stendi mpya ya Mabasi Kizumbi.
Makabidhiano hayo yamefanyika leo Julai 21,2025 kwenye maeneo ya ujenzi wa miradi hiyo, na kushuhudiwa na viongozi mbalimbali wa serikali,Chama pamoja na wananchi.
Katambi akizungumza kwenye hafla hiyo,amesema ujenzi wa stendi hiyo mpya na ya kisasa,itakwenda kuongeza mzunguko wa fedha, pamoja na kutoa ajira nyingi kwa vijana na kuinua uchumi wa wananchi wa Shinyanga.
Amemtaka Mkandarasi ambaye anatekeleza miradi hiyo, kwamba atoe kipaumbele kuwapatia ajira wazawa hasa wakazi wa Jimbo la Shinyanga, ili wapate kunufaika na miradi hiyo,pamoja na kununua vifaa vya ujenzi kwenye maduka yao.
“Tunataka bilioni 26 zinazotekeleza miradi hii zibaki hapa Shinyanga, kwa kutoa ajira kwa wazawa na ununuzi wa vifaa vya ujenzi kwenye maduka ya wafanyabiashara wa hapa kwetu,”amesema Katambi.
Aidha,ameagiza uwepo usimamizi madhubuti juu ya ujenzi wa miradi hiyo, iwe yenye ubora wa hali ya juu na thamani ya fedha ionekane, na Mkandarasi aikamilishe ndani ya muda wa Mkataba.
Ametoa pia wito kwa wananchi, kwamba waitunze miundombinu ya miradi hiyo, ili udumu kwa muda mrefu, huku akimshukuru Rais Dk.Samia Suluhu Hassani kwa kuendelea kumwaga fedha na kuibadilisha Shinyanga kimaendeleo.
Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Shinyanga Mjini Anord Makombe,amesema amejawa na furaha baada ya kuona Mkandarasi amekabidhiwa “Site” tayari kwa kuanza ujenzi, hasa Barabara ya kwenda Hospitali ya Rufaa ya Mwawaza, kwamba ilikuwa ikimyima usingizi.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga Alexius Kagunze,awali akisoma taarifa ya miradi hiyo,amesema kwamba miradi hiyo ni ya TACTIC na iliibuliwa 2020.
Ameitaja miradi iliyoibuliwa kuwa ilikuwa mitatu 3 kwa ufadhili wa Benki ya Dunia,ambayo ni ujenzi wa Barabara ya Lami kutoka Nguzo Nane- Mwawaza Kilomita 4.6, Stend ya Mabasi Kizumbi, na Ujenzi wa Soko la Matunda Kambarage.
Amesema kwa miradi ambayo itaanza kutekelezwa kwa sasa, ni ujenzi wa Barabara ya Lami Nguzonane- Mwawaza,Stendi ya Mabasi Kizumbi, na Barabara ya Lami kutoka Sinatone hadi Ndala Kilomita 1.6.
Ameongeza kuwa katika ujenzi wa Barabara hiyo ya Lami Nguzonane Mwawaza,pia litatajengwa daraja kubwa eneo la Upongoji na kuliondoa lililopo kutokana na ufinyu wake, pamoja na kujengwa uzio katika shule ya Msingi Ndala “A”.
“Gharama zote za miradi hii ni sh.bilioni 26, na utekelezaji wake ni miezi 15 na muda wa matazamio miezi 12, na Mkataba wake ulisainiwa Juni 26,2025 Jijini Dodoma,”amesema Kagunze.
Mkandarasi ambaye anatekeleza miradi hiyo kutoka Kampuni ya SIHOTECH Harson Mchau ambaye ni msimamizi wa miradi,ameahidi kuwa wataitekekeza kwa ubora wa hali ya juu na kuikamilisha ndani ya muda wa Mkataba.
TAZAMA PICHA👇👇
Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Shinyanga Mjini Anord Makombe akizungumza.
Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini Patrobas Katambi,ambaye ni Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu,Kazi,Vijana,Ajira na watu wenye Ulemavu akizungumza.
wa Jimbo la Shinyanga Mjini Patrobas Katambi,ambaye ni Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu,Kazi,Vijana,Ajira na watu wenye Ulemavu akizungumza na Mkandarasi.
Mkandarasi ambaye anatekeleza miradi hiyo kutoka Kampuni ya SIHOTECH Harson Mchau,akizungumza.
Mkurugenzi wa Manispaa ya Shinyanga Alexius Kagunze akizungumza.
Makabidhano site ya ujenzi wa miradi ya Stendi ya Mabasi Kizumbi na Barabara ya Lami kwenda Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Shinyanga iliyopo Mwawaza yakiendelea.